Monday, March 13, 2017

WEMA SEPETU ACHAFUA HALI YA HEWA DODOMA, WAJUMBE WAKONGWE WA CCM WAPANGA KUMRUDISHA KIMAFIA, BONGO MOVIE YAPASUKA VIPANDE VIPANDE, MASHABIKI NJIA PANDA…!




Na Pazia Jeusi. Tanzania
Msanii wa Bongo Movie anayedaiwa kuwa na  wafuasi wengi kuliko msanii yeyote Tanzania Wema Sepetu amechafua hali ya hewa Mkoani Dodoma kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo baadhi ya wajumbe katika mkutano huo wameonesha kusikitishwa kukosekana kwa Wema Sepetu kwenye ziara ya wasanii walikwenda Dodoma.

Wasanii hao waliotambulishwa katika mkutano huo na  Humphrey Polepole katibu mwenezi wa ccm na baadae wasanii hao kupongezwa na Rais John Magufuli kama ni wasanii wazuri.

Mwandishi wetu wa Pazia Jeusi ambaye alijipenyeza katika  ziara ya wasanii hao alisema kuwa pengo la Wema lilijidhihilisha wazi kwani msanii huyo  ni kipenzi cha  wajumbe wengi wa CCM kutokana na mvuto mkubwa aliokuwa nao katika jamii.

Habari zaidi ziliendelea kusema kuwa wajumbe wengi walionekana kumzungumzia Wema  muda wote, huku wakisema kuna haja ya kufanya michakato kabla ya mwaka 2020 kumrudisha CCM Wema Sepetu.

Mwandishi aliendelea kusema “ Naweza kusema ukweli msema kweli mpenzi wa MUNGU kama ambavyo huwa anapenda kusema Rais wetu, Wema Sepetu amedhihisha kama ana nyota kali wajumbe wengi wa CCM wanampenda sana”. Alisema mwandishi wetu wa Pazia Jeusi

Wana Ccm hao walifika mbali na kusema wanafahamu chanzo cha Wema kuondoka CCM ni utofauti wa  kiongozi mmoja wa Mkoa lakini kwa vile wamegundua hilo watahakikisha wanamrejesha nyumbani kabla ya uchaguzi mkuu ujao, wanaamini aliamua kwenda CHADEMA kwa jazba tu za kiongozi huyo wa mkoa.

Kuhama kwa Wema Sepetu na kutua chama pinzani kumeivuruga Bongo Movie na kwa sasa kama imepasuka vipande vipande ambapo mamilioni ya wafuasi wa Wema ambao awali walikuwa chama alichokuwa hivyo wapo waliomufuata na wapo waliobaki.

Source: Pazia Jeusi-Tanzania

 


0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king