Thursday, June 23, 2016

KASHFA NZITO!!!, BONDIA MAARUFU TZ MBARONI KWA KUKUTWA NA KETE 300 ZA BANGI NA MIRUNGI, ATUMIA VIBAYA JINA LA MH MAKONDA ILI POLISI WAMUACHIE, POLISI WAMKAMATA KIMAFIA, AFANDE MAKOMEO APONGEZWA NA WANANCHI..!

  Hapa Bondia Dulla Mbabe akimuomba D/c1090 Thausen Mwamba maarufu Makomeo amuachie huru kwani kama taarifa hizo zitawafikia viongozi wa chama cha ngumi kinachomuongoza atafungiwa hali inayoweza kumuua njaa.

  Bondia Dulla Mbabe kushoto akiwa na Mada Maugo siku walipopima uzito kwa ajiri ya pambano lake.
Mheshimwa Makonda ambaye jina lake limetumiwa vibaya na Bondia huyo ili Askari  D/c1090 Thausen Mwamba maarufu Makomeo  amuachie huru kwa kosa hilo



  Kote za bangi na mirungi anazodaiwa kukutwa Bondia Dulla Mbabe.
  D/c1090 Thausen Mwamba maarufu Makomeo akimbana kwa maswali Dulla Mbabe ambae amevishwa pingu kituoni hapo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar, Simon Sirro
 Rais wa chama cha ngumi za kulipwa Tanzania TPBC (Tanzania Professional Boxing Commission) Chaurembe
 Rais wa Chama cha Ngumi za KUlipwa TPBO Yasin Abdalah
Rais Wa PST Emanuel Mlundwa


Na Zainabu Khatibu-Maskanibongotz

Katika hali ya kushtua Bondia maarufu wa uzito wa juu Tanzania anayefahamika kwa jina la Dulla Mbabe anashikiriwa na Jeshi la Polisi Kanda ya Kinondoni kwa tuhuma za kukutwa na Mirungi na kete zaidi ya 30 za bangi.

Tukio hilo la aina yake lililotokea maeneo ya uwanja wa mpira uliopo Mwanyamala Jijini Dar saa 2:30 za usiku wakati polisi hao wakiwa kwenye msako mkali wa kupambana na uharifu ndipo na Dula alipokutwa eneo hilo. 
Mmoja wa askari aliyeshiriki kumkamata Dulla alisema siku hiyo wakiwa kwenye patro ili hali wakijua uwanjani hapo wahuni wengi hupenda kukaa mara baada ya mazoezi ya mpira ndipo mkuu wa oparasheni kata ya  Makumbusho Kopro Makomeo toka kituo cha Polisi Mwananyamala  alipopanga vijana wake kuzunguka uwanja huo kabla ya kuvamia.
Mashuhuda wa tukio hilo wameieleza Maskanibongotz kwamba baada ya Mkuu huyo wa Oparesheni  huyo kuweka sawa vijana wake ambao wengi ni Polisi jamii wenye mazoezi makali ya michezo yote walipoanza kuvamia eneo hilo, baadhi ya wahuni walifanikiwa kuwatoka Polisi hao kumuacha Dulla, ambaye pamoj na kujaribu kukimbia alinasa katika mikono ya D/c1090 Thuasen Mwamba maarufu kama Makomeo mbaye yupo fiti kila idara alifanikiwa kumpiga mtama uliompaisha kimo cha Ng'ombe na kudondokea kiuno.
Pamoja na mtama huo, lakini Dulla alifanikiwa kunyanyuka na kukimbia hadi nje ya uwanja na kutupa mirungi lakini baada ya muda kutaka kujifanya amewazoea Polisi akarudi na kuanza kuwahoji Polisi nani aliyempiga Mtama, kitu ambacho kiliwafanya Polisi hao kumuuliza kwa nini alikimbia kama si Mharifu, lakini kama alihisi amewaweza Mapolisi, Dulla alizidi kuwajia juu Polisi na kuwatishia kuwapiga up cut za chembe, huku wahuni wengine nao wakipata nguvu ya kurudi uwanjani hapo na kuwazunguka Polisi.

Lakini ili kuweza kuweka hali sawa askari mmoja alitoa bastola ambayo  ilisaidia kuwasambaratisha Wahuni wote ambao walirudi kuhakikisha wanakabiliana na Polisi hao huku nguvu wakizipata kutoka kwa Dulla ambaye baada ya tukio hilo alibaki tena peke yake na kutiwa Mbaroni pamoja na kujifanya kutishia kwamba yeye na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni marafiki kitu ambacho kilizidi kupandisha hasira  D/c1090 Thausen Mwamba maarufu Makomeo  ambaye kwa kushirikiana na vijana wake walifanikiwa kumvisha pingu Bondia huyo huku  anawatishia askari hao kama kuna kazi anataka kufanya na Mheshimiwa Makonda hivi karibuni ya kuchangia madawati kwa kucheza pambano lake na mmarekani. 
Tukio hilo liliendelea kuwa na sekeseke kwani baada ya kufunguliwa Pingu walipofika kituo cha Polisi Mwinyijuma, Dulla alifanikiwa kuwatoka Polisi hao lakini walifanikiwa kumkamatia eneo ya Kapakabana na kumpeleka moja kwa moja kituo cha Polisi cha Oysterbay na kumfungulia OB/RB/11362/16, kwa kosa la kupatikana na kosa la Bhangi na Mirungi.
Gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na Bondia huyo wakati akiwa kituo cha Polisi CCM Mwinyijuma, ambapo bondia huyo alikana kukutwa na bangi hizo,pia gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni ili aweze kuzungumzia tukio hilo lakini  Kamanda huyo alikuwa kwenye kikao na kuomba atafutwe baadaye hadi tunakuletea taarifa hizi bado tulikuwa hatufanikiwa kumpata Kamanda huyo.

Aidha Wananchi mbalimbali wamezungumzia tukio hilo na kulaani vikali kwa bondia huyo kukutwa na madwa hayo, ila la pili kilichowasikitisha ni kutumia vibaya jina la Mheshimiwa Makonda na kuamini kama akisikia taarifa hizi na yeye atachukua hatua kali za kinidhamu kwani kujuana na Mheshimiwa isiwe chanzo cha kuvunja sheria za nchi na wanaamini pia chama cha ngumi kinachomuongoza bondia huyo pia nao watachukua hatua kali za kisheria dhidi ya bondia huyo itakapobainika kama kweli ametenda kosa hilo.

Wananchi walioshuhudia tukio hilo wakimuomba Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Paul Makonda kumtizama kwa jicho la tatu kwa kumpongeza Afande mwenye namba D/c1090 Thausen Mwamba maarufu Makomeo kwa ujasiri wa kumkamata Bondia huyo licha ya kumtishia kama yeye na Makonda ni  ndugu ili wasimkamate, lakini afande huyo alimkazia hadi kumfikisha kituoni na kumfungulia mashtaka.

 Source: Maskanibongotz.

 

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king