Saturday, March 11, 2017

MWANAMUZIKI MR BLUE APIMANA MISURI NA JESHI LA POLISI, ASHUKA NA NDEGE NCHNI KENYA AKITOKEA NJE AINGIA NCHINI KIMYA KIMYA, AISHI KAMA DIGI DIGI PAZIA JEUSI LINAKUPA A-Z...!

 KAMANDA SIRRO VS RC MAKONDA
MWANAMUZIKI MR BLUE.

Na Mwandishi wa Pazia Jeusi- Tanzania
Mwanamuziki wa bongo flava  Herry Sameer aka Mr Blu ambaye hivi karibuni alitajwa kati ya  watu wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya  amerejaea nchini kimya kimya na sasa imeelezwa anaishi kama digidigi kukwepa mkono wa Serikali.
Habari za uhakika zilizothibishwa na matandao huu wa habari za uchunguzi wa Pazia Jeusi "Fichua" umegundua kuwa mwanamuziki huyo yupo nchini na alirejea hivi karibuni toka nchi za nje alikokuwa ameenda kwa kazi isiyojurikana.

Hata wakati Mkuu wa Mkoa anataja majina ya wanamuziki wanaodaiwa kujihusisha na madawa ya kulevya ile kwa kutumia ama kuuza na yeye jina lake lilitajwa  hivyo wakati wenzake wakiwekwa lupango yeye alikuwa nje ya nchi.

Pazia Jeusi "Fichua" ilipata taarifa za mwanamuziki huyo kurejea nchini kwa siri huku ukielezwa kuwa mwanamuziki huyo alishuka na ndege nchini Kenya kisha akapanda basi hadi kufika Dar kwa siri kubwa kwa kuogopa Polisi.

Hata hivyo cha kushangaza mwanamuziki hadi sasa hajaenda kuripoti kituo cha Polisi cha kati kama alivyotakiwa na Mkuu wa Mkoa licha ya habari zake kuvuja kama hivi kuwa yupo nchini hali inayoonesha kama  amelitunishia misuri Jeshi la Polisi.
Mtandao huu wa Pazia Jeusi uliwasiliana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum kutaka kujuwa kama mwanamuziki huyo alisharipoti kituoni kama alivtakiwa ama laa, ambapo simu ya Kamanda Sirro iliita bila mafanikio hadi habari hii inaruka hewani muda huu.
Herry Sameer aka Mr Blu imedaiwa kwa sasa amejificha katika Hotel ya Itumbi, nyumbani kwake hata ukienda humkuti.
Source: Pazia Jeusi-Tanzania 

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king