Na Livingstone Mkoi- Maskanibongotz
Wananchi wa mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa wanaoishi
kwenye mgogoro wa ardhi kwa zaidi ya miaka kumi na tano sasa wameingia hofu
kuhusu hatma ya makazi yao dhidi ya mafisadi wa ardhi ambao tangu Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda aingie kwenye sekeseke la tuhuma za vyeti
batili.
Wakiongea na waandishi wetu wa mtandao wa Maskanibongotz
wakazi hao wapatao elfu nne walisema
tangu ishu ya Makonda ilipozuka watu hao wanaodai wenye mashamba wamekuwa
wakionekana karibu kila siku wakiwa na magari ya kifahari katika makazi yao
jambo linalowapa hofu kubwa.
Hofu waliyonayo wakazi hao ambao hadi sasa wameshahakikiwa
katika eneo hilo na kubakisha kupewa hati za Serikali tu ili wayamiliki
kihalali makazi yao, wamesema wasi wasi huenda watu hao wenye mashamba ambao “
Mafisadi Ardhi” Wakatumia udhaifu wa matatizo ya Makonda kuwaonea mwanzo jinsi
walivyobomolewa makazi yao bila kibali cha mahakama huku watu kumi na tatuu
wakipoteza maisha.
RC Makonda ndiye aliyekuja kusambaratisha mtandao huo wa
ufisaidi na kufanikiwa kuwaweka huru wakazi hao ambapo awari watu waliokuwa
wameyaterekeza mashamba hayo zaidi ya miaka ishirini na kuacha msitu huku majambazi
wakitumia maficho ya uharifu hadi Mkuu wa Mkoa miaka hiyo Yusuph Makamba
alipoamuru Serikali ya mtaa kugawa eneo hilo.
Watu hao wenye mashamba walijaribu kutumia nguvu kubwa ya
kifedha kuwaondoa wananchi kwa kutumia
Polisi, wenye sialaha, na mabomu, na mabaunsa kwa kuwabomolea hadi kupelekea
wakina mama kujifungua kabla ya muda, huku wengine wakipoteza maisha,
walifanyiwa ukatili huo bila msaada wowote katika utawala uliopita hadi
alipokuja Makonda kurudisha amani.
Makonda alionekana adui mkubwa dhidi ya mafisadi hao kiasi
cha kumchukia kwa kuwatetea wananchi hao wanyonge, katika neo hilo palikuwa
hapaingiriki zaidi ya kuwindana na mishare ya sumu kwa wananchi na bunduki kwa
Polisi, ilifika mahara wakazi hao walipewa kesi
kuwa wao sio raia wa Tanzania kwa lengo la kuwaondoka tu, lakini kipindi
cha kupiga kura wananchi hao waliachwa kwa muda ili wapige kura baada ya
kumalizika kupiga kura waliisoma namba.
Baada ya maongezi na wananchi hao waandishi wetu walifika
ofisi za Serikali ya mtaa wa Nyakasangwe zinazoongozwa na Mtumishi wa Mungu
Peter Bilebela kwa ajiri ya kupata ukweli wa jambo hilo.
Mwenyekiti huyo alianza kuzungumzia jambo hilo “ Kwanza
kabisa niwashukuru ndugu waandishi kwa kufika huku kwetu kujionea hali halisi,
kuhusu hizi taarifa za kuonekana kwa watu hao ndani ya magar ya kifahari ninazo
licha ya kwamba mimi sijafanikiwa kuwaona kwa macho yangu” Alisema
Kiongozi huyo aliongeza kusema” Kwa vile wananchi wangu ndiyo
wapo huko mtaani naamini kabisa taarifa hizo ni za kweli kwani katika mitaa
yetu tunaishi kwa ushirikiano mkubwa hivyo wanapoona kitu tofauti lazima
watanifikishia taarifa hizo” Alisema
Hata hivyo mwenyekiti huyo aliongeza kusema kuwa wananchi
wake kweli wapo kwenye hofu kubwa juu ya hatma ya Makonda ambaye kwao
wanamchukulia kama shujaa kutokana na alichokifanya katika mitaa hiyo kwa
kurudisha amani iliyokuwa imetoweka miaka mingi iliyopita.
Mwisho, Mwenyekiti huyo kwa niaba ya wananchi wake ambao wamekuwa
wakimsumbua kila siku wakiwataka
viongozi wakuu wa nchi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini, Mhe. William
Lukuvi siku moja wafike katika mtaa wao
huo wa Nyakasangwe kata ya Wazo. Kumaliza
mgogoro huo ili wananchi waanze kulipa kodi za viwanja na majengo kwani Serikali inapoteza mamilioni
ya shilingi kwa kukosa kukusanya kadi kutokana na uchelewaji wa kuwapimia
wananchi viwanja na kupewa hatimiliki.
Lakini pamoja na hayo wakazi hao wameomba
Jeshi la Polisi kuweka tahadhari juu ya
watu hao wenye mashamba kwani wakijaribu kufanya jambo kuleta uvunjifu
wa amani hali inaweza kuwa mbaya kwani safari hii hawatokubari kuonewa kama
walivyofanya kwa utawala wa Rais Kikwete na kusisitiza huu ni utawala wa
Magufuli ambao hautaki uonevu na upo kwa ajiri ya wanyonge.
Source: Maskanibongotz
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini, Mhe. William
Lukuvi
0 comments:
Post a Comment