Wednesday, December 14, 2016

NILIAHIDIWA USTAA KAMA NINGETOA RUSHWA YA NGONO KWA MR CHULZ- TRACY MOSHI…!

Msanii Tracy Moshi ”Breen”

Mr. Chuz na Kabula aliyezaa nae mtoto mmoja.

Na Mwandishi Wetu
Msanii mchanga kwenye kiwanda cha filamu Tanzania Tracy Moshi ”Breen” ameibuka na kumwaga mboga jinsi msanii na Director Tuesday Kihangala 'Mr. Chuz' alivyomuaidi ustaa kama angetoa uroda.
Msanii huyo toka Mkoa wa Tanga ambaye ametambulishwa vyema kwenye filamu alizocheza kama filama ya msanii Manaiki Sanga Wake Up, Our Teacher,Behind The Pastor, Ngema na filamu ya kimataifa ya Going Bongo, alisema bila kuwa na msimamo na anachokifanya  'Mr. Chuz' alifanyia udharirishaji huo.
Akipiga stori na gazeti hili hivi karibuni msanii huyo alisema jinsi alivyoshawishiwa kwenda kufanya usahir wa wa moja ya filamu ya Mr. Chuz “ Kaka kwa mara ya kwanza nilipigiwa simu na Mzee Magari akaniambia Mr. Chuz anataufuta wasanii wa dizaini kama yangu hivyo kwa vile mimi nina vigezo nikasema poa ntakwenda huko Jijini Dar” Alisema Breen
Msanii huyo aliendelea kuongea kuwa kutokana nay eye kuwa msanii mwenye ndoto kubwa katika tasinia ya sanaa ya tz basi alifunga safari toka Tanga hadi Dar na moja kwa moja alikwenda Makondo Ccm ndiko zilipo ofisi za msanii huyo.
Baada ya kufika huko Makongo akiwa ameongozana na msanii mwenzake aliyemtaja kwa jina moja la Preshazi na mara baada ya kufika huko alikuta wasanii wengi huki akiitwa mmoja baada ya mwingine na ilipofika zamu yake ya kuingia kwa bosi huyo ndipo alipoanza kumleta mapicha picha.
Breen anasema “ Nilipoingia tu Mr. Chuz alianza kusema mimi ndiye staa wake mpya hivyo wala sihitahi usahiri nimepita moja kwa moja hivyo nitoke nje ila nisiondoke hadi amalize kuwafanyia usahiri sanii wengine” Alisema
Cha kushangaz msanii huyo anasema Mr. Chuz alipomaliza kazi alianza kumletea habari hizo za mapenzi huku akiweka wazi kabisa kama atatoa kiburudisha basi atamfanya kuwa taa wa katika filamu zake , huku akimpigia mfano msani Jini Kabula, na Jack ambao walikubari kutoa uroda lakini amewapa ustaa hadi leo umewasaidia.
Breena anasema alishindwa kukubaliana na matakwa ya Mr. Chuz na kuamua kuondoka lakini jambo hilo akaamua kumueleza Mzee Magari ambaye nae alisikitishwa sana na tukio la msanii huyo kwani tabia kama hizo zimekuwa zikiwakatisha tamaa wasanii wachanga. 
Hata hivyo msani huyo anasema ameamua kuliweka wazi jambo hili ili kuwanusuru wasanii wengi wachanga ambao wamekuwa wakitoa uroda kwa waongza filamu ili wawapatiea nafasi za kucheza filamu zao jambo ambalo sio sahihi.
Baada ya taarifa hizi gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Mr. Chulz kupitia no yake ya kiganjani ili ajibu tuhuma hizi na aeleze kama anamfahamu msanii Breen lakini simu yake iliita bila mafanikio hadi gazeti hili linakwenda mitamboni jana, lakini mtandao huu unaendelea kumsaka Chulz ili ajibu tuhuma hizo ambazo pia zimekuwa zikilalamikiwa sana na wasanii wachanga kwa  Madirectors wengine wanawataka kutoa tamu tamu ndipo wapewe nafasi za kucheza filamu.


Source Maskanibongotz

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king