Saturday, July 2, 2016

MUNGU WA KWELI AJIDHIHIRISHA KWA MCHUNGAJI HUYU, MCHUNGAJ MZOLA ATAKA KULETEWA VICHAA, MATASA, WENYE UKIMWI, KISUKARI, NGUVU ZA GIZA, MAELFU WAZIDI KUMIMINIKA KANISANI KWAKE...!


 Hii ndiyo taswira ya waumini wanaendelea kupokea uponyaji wa kweli toka kwa mchungaji Mzola wa Kanisa la Hosana Ngome ya Yesu lililopo Nyakasangwe Wazo.

 Mchungaji Mzola wa Kanisa la Hosana Ngome ya Yesu akiendesha ibada kwenye Kanisa lake


Na Amina Saidi- Maskanibongotz
Yule mchungaji kiboko ya wachawi nchini Tanzania Mch Mzola wa Kanisa la Hosana Ngome ya Yesu ameendelea kuwaasa wakazi wa Jiji la Dar na hata mikoani kuendelea kumpelekea watu wenye matatizo sugu yaliyoshindikana huko kote hata kwa wachungaji wengine.
Akionge jana kwenye ibada ya maalum ya kumuombea Rais Magufuli,Paul Makonda na Waziri Lukuvi ili kuendelea kuguswa na mgogoro wa ardhi ulioua watu zaidi ya 23 hadi sasa.
Mchugaji Mzola amesema anashukuru kumekuwa na muitikio mkubwa toka kwa wakazi wa Jiji la Dar ambayo wengi wamepokea uponyaji wa kweli na sasa mambo yao yamekaa vyema na Mungu amewabariki.
Mcungaji huyo amesema watu waendelee kuwaleta jamaa zao wenye magonjwa sugu na watapokea uponyaji wasioutegemea kwa maana Mungu wake yeye ni mungu wa kweli na uzima na ni MUNGU asiye babaisha hivyo wote wanahitaji tiba hiyo toka kwake  wafike kanisani kwake matibabu na dozi zake ni bure tu kumpa mungu utukufu tu ndiyo malipo yake .
Mchungaji huyo aliongeza kusema kuwa anaendelea kutoa uwito kwa watanzania wote kuendelea kufika Kanisani kwake ili wapate uponyaji, kwani Kwa Mungu hakuna lisilowezekana, kila magonjwa yote sugu, ugumba, utasa, mikosi ya kushindwa kuolewa/kuona, kuwa na mashaka, hofu ya kifo nk.
Na amesema watkaoshindwa kufika kanisani kwake Kata ya Wazo mtaa  Nyakasangwe wanaweza kumpigia simu kupitia namba hizi 0763-161785/ 0713-161785 na wao watapokea uponyaji huko walipo.  

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king