Monday, July 4, 2016

KASI YA MAKONDA KIBOKO, CHADEMA WAUNGA MKONO MITAA KUPEWA JINA LA MAKONDA KWA HESHIMA NA KAZI NZURI ALIYOIFANYA, UKAWA WAMSHAURI HAYA MEYA KINONDONI...!

 Pichani Mkuu wa Mkoa Dar kipindi akiwa DC Kinondoni akiongea na wananchi wa Nyakasangwe na kuwatia kuhusu Mgogoro huo wa Ardhi na kuahidi kutatua haraka tatizo hilo ili wananchi waishi kwa amani kama wakina ndani ya nchi yao.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob ambaye ameshauriwa na watanzania wengi hasa wakazi wa Jiji la Dar kushirikiana na mheshimiwa Makonda kumaliza tatizo la mgogoro wa Nyakasangwe ambao unaonekana unanuka rushwa zilizowahusishwa baadhi ya  watendaji wa mipango miji Kinondoni lakini pia hata ofisi ya Mkuu wa Mkoa kabla ya Makonda nao wamehusishwa na mgogoro huo kwa kushindwa kusimamia na kumaliza tatizo hilo.
Na Mwandishi Wetu. Wazo
Wanachama wa Chema Wilaya na Kinondoni wameunga mkono maombi ya wananchi wa mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa kutaka mitaa hiyo kuitwa jina la mheshimiwa Makonda na kusema anastahir kwa kazi aliyoifanya.
Wakiongea na maskanibongotz wananchama hao pia wanaunda Ukawa walisema" Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpenzi Makonda anastahiri heshima kwa kazi nzuri aliyoifanya kwenye mgogoro huu wa ardhi" Alisema kijana mmoja ambaye ni kata wa kutupwa wa Chadema
Aidha wananchama hao waliendelea kusema kuwa amani inayooneana sasa Nyakasangwe yenye wakazi zaidi ya elfu tano ni kazi ya Makonda ambaye amefanikiwa kufanya kitu kilichowashinda viongozi kiba " Jamani ili kwa hili hakiaka sisi kama wapinzani tunaunga mkono maombi haya ya mitaa hii kupewa jina la Makonda kwa vile anastahiri hivyo na ili hata vizazi vijavyo vije kutambua mchango  mkubwa uliofanya na kiongozi huyo mpenda haki na mtetezi wa wanyonge" Alisema Mama zainabu
Mheshimiwa Makonda ambaye mara kadhaa katika mikutano yake Nyakasangwe amekuwa akiwatia moyo sana wananchi hasa wakina mama hao na kuwafananisha na Mama yake mzazi lakini pia na maisha aliyokulia mheshimiwa huyo ni hali ya chini hivyo amekuwa akiwambia wakazi hao wasiwe na shaka iko siku maandiko yatatimia na wataishi kwa matumaini huku wakiwa na hati zao.
Wadau mbali mbali wamemshauri Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob kuwa makini na ataarifa anazozipokea toka kwa watendaji wake hasa wa Wazo ambao wamekuwa wakimpa taarifa tofauti juu ya mgogoro huo ambao kimsingi ni kama umeisha, huku kukiwa na taarifa kama viongozi hao wana bifu za kisiasa na mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyakasangwe Mtumishi wa Mungu Pete Bilebela wa CCM.
Sourc: Maskanibongotz

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king