Tuesday, June 28, 2016

KIMENUKA: RAIS MAGUFULI, PAUL MAKONDA NA LUKUVI WAZUSHA HOFU, MAJINA YA MAFISADI ARDHI KATA YA WAZO WANAODAIWA KUUWA WANANCHI WASIOKUWA NA HATIA KUTUA MEZANI KWA MH RAIS. VIONGOZI WA DINI WAWAOMBEA MSAMAHA WENYE MASHAMBA WALIAMUA KUWAACHIA WANANCHI...!

 Mkuu wa Mkoa wa Dar Mheshimiwa Paul Makonda ambaye inadaiwa anataarifa kamili kuhusu mgogoro huo kutokana na mafanikio makubwa aliyofikia ya kuleta amani na mshikamano kwa pande hizo mbili watu wenye mashamba na wananchi wakazi wa maeneo hayo.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akikagua utendaji wa watumishi wa Mipango Miji na Ardhi Wilayani Ilemela., ambapo wakazi wa Nyakasangwe nao wanaimani na Mheshiwa Lukuvi iko siku moja atakuja kufanya maamuzi magumu.
Aliyekuwa kiongozi wa mabaunsa ambaye kwa sasa ni marehemu aliyefahamika kwa jina moja la Chura, picha ikionesha jinsi alivyokatwa mapanga kwenye mgogoro huo wa ardhi uliotokana na mafisadi kutumia mabaunsa hao kuvunja nyumba na wananchi bila kibali halali mcha mahakama na kusababisha vita kubwa na kupelekea vifo vya mabaunsa hao na wananchi.

Dokta John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania ambapo Serikali yake kwa sasa imerusha matumaini mapya kwa wananchi kutokana na utendaji wake kazi wa haki na kuwatetea wapiga kura wake, hali hiyo ikizusha hofu kwa watu wenye fedha waliozoea kuwaone wananchi kwa fedha zao, ambapo jambo hilo kwenye Serikali hii limekuwa gumu huku Rais akiwa mstari wa mbele kupambana na ufisadi wa kila aina, Hali hiyo imeendelea kuwapa matumaini wakazi Wazo mitaa ya Nyakasangwe na kuamini iko siku maandiko yatatimia kwa Serikali kufanya maamuzi magumu ya kuwakamata mafisadi ardhi wote waliofanya uharibifu na kuua wananchi.
 Na Livingstone Mkoi

Utendaji kazi wa haki na uwazi unaofanywa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais  Dk John Pombe Magufuli umeleta matumaini mapya kwa wakazi wa kata ya Wazo kwenye mitaa ya Nyakasangwe na Nyakalekwa wanaoongozwa na Mwenyekiti wao Mch Peter Bilebela ambao kwa muda mrefu  wamekuwa wakipata shida na kujiona kama vile si Watanzania kutokana nak kile kinachodaiwa kukosekana kwa uaminifu kwa baadhi ya watumishi wa Serikali ambao walikuwa wanatumiwa na baadhi ya watu wenye fedha nyingi au maarufu kwa majina ya mafisadi ili kuwaonea wananchi hao huku wakiitwa wavamizi na wakimbizi.

Wananchi hao walikosa imani na baadhi ya viongozi wa Serikali ya awamu ya nne ambao wanadai ni kama walifanikiwa kuhodhiwa na matajiri hao hivyo ofisi ya Mkuu wa Mkoa iliyokuwa inaongozwa na Bw. Saidi Meck Sadiki, ofisi ya Mkuu wa Wilaya iliyokuwa inaongozwa na Mheshimiwa Jordan Lugimbana , Meya wa Kinondoni, Yusuf Mwenda na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mussa Natty, Jeshi la Polisi Kanda Maalum hivyo kushindwa kumaliza tatizo lao la mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wakazi wa mitaa hiyo na watu wanaojiita wenye mashamba hali iliyopelekea badala yake utatuzi kuelemea upande mmoja na ilitumika nguvu kubwa toka Jeshi la Polisi Kanda Maalum lililokuwa likiongozwa na Suleiman Kova  kuwahamisha wakazi hao mara moja kwa amri toka ofisi ya mkuu wa Mkoa kwa madai kuwa watu hao ni wavamizi.


 Zoezi hilo ambalo lilihusisha silaha za moto huku matajiri hao wakihusishwa kugharamia mafuta na posho za zilizonona kwa walioendesha zoezi hilo,kitu ambacho kilipelekea vita kubwa kuibuka na wananchi walichezea kichapo cha mbwa mwizi, huku mali zao zenye thamani ya mabilioni ziliharibiwa vibaya, watoto wakikosa pa kujificha huku watu zaidi ya kumi na tatu wakipoteza maisha kwenye mapambano hayo ya ugomvi wa ardhi hivyo kupelekea kuibukakwa uhasama  kati ya raia na Polisi, watu wa manispaa kiasi cha kufanya eneo hilo lile gumu kuingilika na jeshi la Polisi bila kuwa na silaha za moto kwani Wananchi hao walikuwa wanatamani kuwadhuru.

Maskani linatambua kuwa mtu aliyemaliza mgogogro huo ni Mheshimiwa Paul Makonda kipindi hicho akiwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambapo alifanikiwa kurudisha hali ya amani kiasi cha kuwashangaza hata viongozi wengine waliokuwa wameshindwa kufanya hivyo ambapo hadi sasa wakazi hao wameendelea na shughuri zao za ujenzi wa taifa licha ya kwamba bado wakazi wengi hawajapatia hati miliki za viwanja wanavyoishi kutokana na baadhi ya watu wanaojiita wamiliki  kuendelea kung'ang'ania kama wana haki na maeneo hayo ambayo sio mashamba tena kama wanavyodai bali yameshakuwa makazi ya watu. 


Hata hivyo zoezi la mwisho kwenye mgogoro huo ilikuwa kwa wakazi hao kuhakikiwa majina na viwanja wanavyooishi, lakini kuna baadhi ya watu waliokuwa kwenye idadi ya watu wanaosema makazi hayo yalikuwa mashamba yao ambao ni Rajabu House na Bwana Pius wao kwa moyo mkunjufu walitangaza kuachana na mgogoro huo hivyo maeneo yao ambayo yalikuwa msitu mkubwa kabla ya wananchi kupewa na Mkuu wa Mkoa mstaafu Mheshimwa Yusuph Makamba wayaendeleze baada ya kuwa maficho ya wezi, hatua ambayo imepongezwa na watu wengi wakiwemo viongozi wa dini na vyama vya Siasa kwa vile taarifa za ndani kabisa zinadai vyombo vinavyohusika na mambo ya usalama kwa sasa vinaendelea na uchunguzi juu ya jambo hilo na kubaini watu hao wenye mashamba walipata wapi mamlaka ya kumiliki na hata kusababisha vifo vya watu na kuharibu mali zao.

Wakiongea na maskanibongotz viongozi hao wa dini waishio eneo hilo ambao na pia ni wahanga wa kuvunjiwa, Mchungaji Mzola wa Kanisa la Hosana Lililopo Nyakasangwa alisema " Uonevu uliofanyika kwa wakazi hawa wa Nyakasangwe pamoja na damu zao kumwagika sisi kama watumishi wa MUNGU tulisha mwomba yeye atoe hukumu kwa wote waliohusika na hili jambo, lakini tunamuomba Rais wetu mtukufu Mheshimiwa John Pombe Magufuli kuwasamehe hawa watu wenye mashamba waliosamehe vita hii ya mgogoro wa ardhi kwa vile tayari wametubu madhambi yao" Alisema Mchungaji Mzola.

Aidha  Shekh Saharif Khamis ambaye tangu mgogoro huo uanze amekuwa akiombea dua amani ili watu wasimwage damu, amefurahishwa na watu wenye mashamba waliosamehe maeneo hayo,  ‘Utendaji kazi wa haki unafanywa na Rais John Pombe Magufuli, Mheshimiwa Paul Makonda na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi huenda ndiyo uliopelekea baadhi ya watu hao wanajiita wenye mashamba kuamua kuachana na mgogoro huo kutokana na misimamo mikali ya viongozi hawa wapenda haki, ambapo hadi sasa kimya chao kuhusu sakata hili la ardhi ambapo Mheshimiwa Makonda ana picha nzima ya mgogoro huo kutokana na kamati yake aliyoiunda wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni huenda kikawa na mshindo mkubwa siku yeyote maamuzi magumu yanaweza kufanyika kumaliza mgogoro huo wa ardhi ili wananchi waendelee kurudisha imani kwa Serikali yao. 

Source: Maskanibongotz.



0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king