Wednesday, July 6, 2016

BAADA YA KUAPISHWA JANA: MKUU WA WILAYA KINONDONI AAPA JAMBO ZITO , AANDALIWA MAPOKEZI YA KUFA MTU MITAA YOTE KUSIMAMA KWA MUDA...!

 Mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Salum Hapi Ali ameapa kufuata nyayo za Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kwenye kutatua tatizo la migogoro ya ardhi na tayari ana kamati maalum inayojumuisha watu wa mipango miji,maafisa ardhi hivyo kazi hiyo itaanza mara moja, DC huyo aliongea hayo juzi wakati akiapishwa tayari kuanza majukumu yake kwenye Wilaya hiyo yenye wajanja wajanja wengi hasa wenye fedha ambao wamekuwa wakiwaonea watu wanyonge. Lakini hata hivyo kwa sasa Jiji zima la Dar kwa  macho yote wameyaelekeza Kata ya Wazo kwenye mitaa ya Nyakasangwe na Kaza Roho ambako RC Makonda tayari alikuwa amefikia mahara pazuri za kumaliza mgogoro huo uligharimu maisha ya watu zaidi ya 13 huku wakina mama wakijifungua kabla ya siku zao na watoto zaidi ya 250 kupoteza masomo yao kutokana na watu wanaojiita wenye mashamba kutumia pesa zao kuwashika viongozi wa Polisi na wilaya kisha kujichukulia sheria mikononi bila kibali cha mahakama na waliweza kwenda kuvunja tu nyumba za watu na kuwatia umasikini mkubwa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyakasangwe na Kazaroho Mch Peter Bilebela akiongea na maelfu ya wananchi wa mtaa wake waliokuwa wanamsubiri Makonda kwenye moja ya mikutano yake ya kuwatete wananchi wanyonge.
Rais Dk John Pombe Magufuli ameombwa pia kuangalia kwa jicho la tatu mgogoro wa Nyakasangwe na kuwaongezea meno RC Makonda, RC Kinondoni, kwani ndani yake kuna baadhi ya watumishi wa Serikali walihusika kuwaonea wapiga kura wake hali iliyopelekea wakazi hao zaidi ya 5000 kukosa imani na Serikali yao hadi hivi karibuni alipokuja Makonda kurudisha imani kwa wakazi hao na kubaini kama wapo baadhi ya watendaji toka Mipango Miji Manispaa ya Kinondoni walihusika kwa kiasi kikubwa kuwaonea wananachi hao wanyonge kiasi cha kuwaita wakimbizi ili waondolewe maeneo hayo waliyopewa na Mkuu wa Mkoa Miaka mingi iliyopita baada ya msitu huo kuwa tishio kwa usalama wa wananchi.

 Marehemu Chura ambaye alikuwa kiongozi wa mabaunsa aliyekuwa upande wa wenye mashamba kwenye harakati za kuwaondoa wananchi hao wa Nyakasangwe  kinguvu, hali iliyopelekea vita kubwa kuibuka huku baunsa zaidi ya watatu kufariki kwenye mapambano hayo licha ya kwamba walijitahidi kwa kukimbia lakini mwisho wa siku waliishiwa pumnzi kisha wakakamatwa na kuanza kukatwa katwa mapanga
RC Makonda alivyopokelwa na Mabango yakimtaka kuondoa mtandao wa ufisadi kwenye kitengo cha Ardh Kinondoni ambao wanadaiwa kuwa chanzo cha mgogoro huo kwa kuhodhiwa na wenye mashamba wenye pesa chafu.
Na Sakina Sahaban
Mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Salum Hapi Ali ameapishwa juzi tayari kuanza kuitumia wilaya ya Kinondoni huku macho, masikio ya wakazi wa Jiji yakielekezwa Kata ya Wazo mitaa ya Nyakasangwe na Nyakalekwa ambako kuna shida sana huku rekodi zikionesha ndiko kulikopoteza maisha ya watu wengi kwenye mgogoro wa ardhi.
Watu wanaodaiwa kuwa wenye mashamba wamekuwa na nguvu kubwa ya kifedha na wameshika idara zote kabla ya Makonda hajawa DC Kinondoni na alipokuja kidogo nguvu hiyo ya uonevu wa wazi ilianza kufifia kutokana na msimamo mkali wa Makonda wa kutetea wanyonge.
Hata hivyo watanzania wengi wanaimani na Mheshimiwa Ali Salum Hapi Ali na wanaamini kuwa atawasaidia wakazi hao wa Nyakasangwe na Manispaa ya Kinondoni kushirikiana na Meya wake watawapatia wakazi hao hati halali za viwanja hivyo walivyopewa kihalali na Serikali ya Mkoa chini ya Makamba.
Pia kauri hiyo ya Mkuu wa Wilaya aliyoitoa imewapa matumaini wakazi wa Nyakasangwe huku wakiahidi kumuandalia mapokezi makubwa siku ya kwanza kufanya ziara ya kikazi kwenye mitaa yao huku wakiwa na matumaini makubwa na kiongozi huyo kijana.
Source; Maskanibongotz 

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king