RC MAKONDA KIPINDI AKIWA MKUU WA WILAYA KINONDONI AKIWA AMEZUNGUKWA NA MABANGO YENYE JUMBE MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA KUONDOA UFISADI WA ARDHI KWENYE KITENGO CHA MIPANGO MIJI KINONDONI AMBAO WALISHRIKIANA NA MAFISADI KUFANYA UHARIBIFU MKUBWA WA MALI BIKA KIBALI CHA MAHAKAMA HUKU WATU ZAIDI YA SABA WAKIPONEZA MAISHA.
Na Livingstone Mkoi
Nyota ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda imeendelea kung'ara baada ya wakazi wa kata ya Wazo mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa kuiomba Manispaa ya Kinondoni kuruhusu mitaa hiyo kuitwa jina la Makonda kutokana na kazi kubwa aliyoifanya wakati akiwa mkuu wa Wilaya hiyo.
Wakiongea na Maskanibongotz/ Sadicktv wakazi wa maeneo hayo kwa nyakati tofauti walisema ‘Mheshimiwa Makonda amefanya jambo kubwa sana kurejesha amani iliyokuwa imepotea hadi kusababisha maafa kwenye mgogoro wa ardhi katika eneo letu’ , eneo hilo awali lilikuwa na vita ya wakazi na watu wanaojiita wenye mashamba ilikuwa vita ya kutumia siraha za jadi kama mishale, mapanga na visu baina ya watu wanaosadikika kumiliki maeneo makubwa na wakazi ambao wamekuwa wakiishi hapo kwa muda mrefu,kitu ambacho kilipelekea hata jeshi la Polisi kushindwa kuthibiti kwa wakati.
Baada ya kuteuliwa Ukuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ziara yake ya kwanza ilikuwa eneo hilo ambapo siku ya kwanza alifika katika eneo hilo na gari zisizopungua saba za Polisi na kufanya mkutano katika viwanja vya Shule ya msingi ya Wachina ambapo aliwaaahidi wakazi hao kuwa atapigana kufa na kupona kuhakikisha wakazi hao wanapata haki yao ya kupata ardhi lakini na kurejesha amani iliyokuwa imepotea.
Makonda alianza kuunda kamati iliyoshirikisha sehemu tatu, moja ilikuwa ni ya watu wanaojifanya wenye mashamba, mbili ya wakazi wa eneo hilo na tatu iliyokuwa chini yake na baadaye alikaa chini kukubariana wafanye uhakiki kwanza wa maeneo hayo ili kubaini ni kweli watu hao wenye mashamba wanachokisema kuhusu ukubwa wa maeneo yao ni sahihi.
Zoezi la kuhakiki lilianza mwaka jana lakini ikabainika madudu makubwa kwani watu wanaosema hayo ni mashamba yao walionekana kufanya udanganyifu wa hali ya juu kwa kile kilichoonekana kwamba wamejiongezea maeneo kinyemela tofauti na vile ambavyo inaonyesha katika michoro, hivyo kupelekea kazi sasa kuwa rahisi kugawa haki kwa wakazi wa eneo hilo.
Hata hivyo zoezi hilo kwa sasa limesimama tangu Makonda apande cheo huku wananchi wote wa eneo hilo masikio yao, macho yao na akili zao zipo kwa Mkuu huyo wa Mkoa ambaye ndiye wanayemtegemea kutatua tatizo hilo, huku wakiamini ya kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watu hao wenye mashamba kwa mambo matatu, la kwanza walisababisha mauji ya watu saba wakati wa mapambano kipindi walichokuja kuvunja eneo hilo, na suala jingine ni nani aliyewapa mamlaka ya kuwavunjia watu nyumba zao pamoja na kuharibu mali zao zenye thamani ya mabilioni ya pesa na la mwisho uongo wa kumdanganya Makonda na vyombo vya sheria.
Kwa sasa hali ni shwali katika eneo hilo, kinachosubiriwa ni hatua zichukuliwe dhidi ya waharibifu, lakini amani ambayo wanaipata Wananchi wa eneo imewafanya watoe ya moyoni kwamba pasipo Paul Makonda hawajui mpaka leo wangekuwa katika hali gani ‘Tulijiona si Watanzania tena, Makonda ametufanya tufurahie amani ya nchi yetu, kwa sasa tunaishi kwa amani sana, tunaomba Serikali itusikie, hatuna cha kumpa Makonda, lakini ni heshima kwetu kuona eneo hili linapewa jina lake, hii itatosha kuwaambia watu wote na vizazi vijavyo kazi nzuri aliyotufanyia Kijana huyu’, walisema Wazee wa eneo hilo.
Katika hatua nyingine Viongozi wa Dini wa eneo hilo, wamesema ya kwamba kuna wakati Mungu anawatumia watu wake kuokoa, kwa nyakati tofauti Viongozi hao wamesema unaposoma maisha waliyoishi mitume na manabii, utapata kuona jinsi ambavyo walitumwa na kupambana pale inapotokea kwamba eneo fulani linakosa amani, eneo hili awali Mkuu wa Mkoa aliyepita Mecky Sadick alikuja lakini hakuweza kumaliza tatizo, tumeona alichofanya Paul Makonda, tunasema huyu alitumwa kuhakikisha anarejesha amani ya Nyakasangwe na Nyakalekwa, tunamuombea kwa Mungu na hakika anastahili heshima hii ambayo wakazi wa eneo hili wameamua kumpa, alisema Mchungaji Mzola wa Kanisa la Mlima Sayuni Nyakasangwe.
Source Maskanibongotz
0 comments:
Post a Comment