Saturday, June 4, 2016

RC MAKONDA AWASHANGAZA WATU KWA MAMBO YAKE ANAYOYAFANYA, WAMSHAURI KITU RAIS JOHN POMBE MAGUFULI KUTOKANA NA TABIA HIYO YA MKUU WA MKOA..!

 Mkuu wa Mkoa wa Dsm Mheshimiwa Paul Makonda
Umati wa mashabiki ukimsikiliza Mheshimiwa Paul Makonda ambaye hayupo pichani.
Na Livingstone Mkoi
 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr Pombe John Magufuli hakufanya kosa kumchagua Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar kutokana na utaofauti wake na wakuu wa mikoa mingine.
Hilo limedhihilika jana kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama katika hali isiyotarajiwa Mheshimiwa Paul Makonda alijichanganya na vijana wa bodaboda na bajaji pamoja na mashabiki wa muziki wa Singeri waliokuwa wamefurika viwanjani hapo hadi kukosekana nafasi ya kupita.
Makonda ambae ana histori ya kutokupenda mbwembwe kwenye misafara yake tofauti na wakuu wengine wa Mikoa ambao hupenda kuandamana na misafara ya polisi kwa mbwembwe aliingia kwenye viwanja hivyo jioni majira ya saa kumi na nusu huku akiwa na mlinzi wake tu.
Kitendo hicho cha mkuu huyo wa mkoa kujichanganya kwenye show za hali ya chini kimewashangaza watu na kusema Makonda anatakiwa kuwa mfano kwa wakuu wote wa Mikoa kuiga tabia kama yake ya kuwajar watu wote bila kujari wa hali ya juu ama ya chini.
Kutokana na mambo hayo ya Makonda kuwa mfano mzuri kwenye jamii, watu mbalimbali waliofika uwanjani hapo kwenye onesho la Komaa Concert lililohudhuliwa na watu wasiopungua elfu 45 walimshauri Mheshimiwa Rais kwenye uteuzi wake wa wakuu wa Mikoa ateue watu wenye sifa kama Makonda asiyekuwa na makuu.
Ujio wa Makonda uwanjani hapo uliwashuta hata maafisa wa Polisi toka kituo cha Polisi Oysterbay ambao hawakutegemea kama Mheshimiwa Makonda angeweza kuja uwanjani hapo kujichanganya na vijana wa hali ya chini, ghafra walimuona tu akitunda dunda viwanjani hapo akiwa na mkuregenzi wa kituo cha E-fm Radio Bwa Francis Siza "Majey"  

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king