Monday, December 14, 2015

MWANDISHI WA HABARI AOTA UWAZIRI KWA RAIS MAGUFULI, ASEMA ANAMUDU NAFASI YOYOTE KAMA IKITOKEA MHESHIMIWA RAIS AKIMKUMBUKA...!

 Mwandishi wa habari maarufu nchini Bossngasa akiwa maeneo ya viwanja vya bunge hivi karibuni kwenye michakato flani na waheshimiwa wabunge na mawaziri
 Boss ngasa kwenye muonekano.
Na Mwandishi wetu- Dodoma
Mwandishi wa habari maarufu nchini Bossngasa ameijitokeza na kuonesha hisia zake kwa mheshimiwa Rais kama atamkumbuka hata Uwaziri flani kwenye nafasi zilizobaki ambazo hadi sasa Mheshimiwa hajachagua.

Akiongea na maskanibongotz, Ngasa alisema " Naweza kusema kuwa mimi ni kijana msomi na ni hadhina ya taifa hili hivyo kwa uwezo wangu wa kudadavua mambo ya kijamii nadhani Mheshimiwa Rais anaweza kunikumbuka hata nafasi  moja tu ili niwaonesha watanzania kama mimi naweza" Alisema Ngassa
Aidha Ngasa ambae ni rafiki kipenzi na Mbunge na Naibu waziri Mh Antonie Mavunde  amesema anampongeza Mh Rais kwa kumchangua Mh Mavunde kuwa Naibu Waziri kwani hakufanya makosa Mavunde ni mpiganaji na msomi mwenzake mwenye kujitambua.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king