Sunday, December 13, 2015

MASIKINI WEEH: PRODYUZA WA WEMA SEPETU HALI TETE NI YULE ALIYETIMULIWA KWA KASHFA YA KUFANYA NGONO KWENYE MAGARI YA WEMA, MASHABIKI WAMUOMBEA KWA WEMA AMSAMEHE ILI KUMUOKOA, ANASWA KWA MSANII MANAIKI SANGA AKIOMBA KIBARUA..!

 Aliyekuwa Prodyuza wa Wema Sepetu, Chidy enzi hizo akiwa kwenye ofisi za Wema zilizokuwepo Mwananyamaka Komakoma, ambapo watu wa karibu na Prodyuza wameumbiwa mtandao wa maskanibongotz kuwa wanamuomba Wema amsamehe Prodyuza wake huyo wa zamani kwani hali yajke kiuchumi ni mbya na sasa anatia huruma, hali iliyomfanya akampigie magoti msanii Manaiki Sanga kwa kumuomba kibarua kwenye studio yake ya Manaiki Production iliyopo ndani ya Itumbi Hotel
Msanii na Mkurugenzi wa kampuni ya Manaiki Production, Manaiki Sanga  akiwa mbele ya gari yake mpya aina ya Range Rover
Chidy enzi hizo akiwa na boss wake Wema Sepetu
Na Mwandishi wa Maskanibongotz
Aliyekuwa Prodyuza wa Wema Sepetu aliyefahamika kwa jina moja la Chidy inadaiwa yupo kwenye hali mbaya kimaisha kutokana na ukata wa kufa mtu tangu alipotimuliwa na bosi wake Wema Sepetu.
Habari za uhakika zilizonaswa na mtandao huu wa maskanibongotz  zilisema kuwa Chidy tangu afukuzwe kazi kwa kashfa ya kufanyia ufuska magari ya Wema amekuwa akiishi maisha magumu wakati mwingine hukaa siku tatu bila kula.
Akiongea kwa sharti la kutotajwa jina lake mtu wa karibu na Prodyuza huyo alisema " Kaka jamani ebu muombeeni Chidy kwa Wema amrudishe kwenye kampuni  atakufa njaa huyu, kiukweli hali yake inatia mashaka sana" Alisema mtu huyo
Hata hivyo habari zaidi zilisema kuwa kwa sasa prodyuza huyo amekuwa akishinda Itumbi Hotel kwa ajiri ya kuomba kibaru kwa msanii Manaiki Sanga kwenye Production yake na hivi juzi alinaswa akiwa mapokezi akisinzia baada ya kumsubiri Manaiki kwa muda mrefu.
Maskanibongotz ilifanyajitihada za kuongea na Chidy kupitia simu yake ya kiganjani ambapo simu hiyo iliita bila mafanikio hadi habari hii inawafikia wasomaji wetu makini.
Source: Maskanibongotz

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king