Monday, December 28, 2015

KATA YA WAZO YAKUMBWA NA MSHTUKO MKUBWA, MAMBO ANAYOYAFANYA MCHUNGAJI HUYU YATISHIA AMANI, MWENYEWE AONGEA HAYA......!

Mtumishi wa Mungu Mch: Mzola wa Kanisa la Hosana Msigani Linalotambulika kama Ngome ya Yesu akiwa kweenye ibada

 Baadhi ya waumini wakiwa Kanisani hapo kwa ajiri ya kupokea uponyaji wa ajabu


 Ushuhuda: Mama akitoa ushuhuda jinsi mwanae alivyopata uponyaji baada ya kuugua ghafra kiasi cha kupoteza fahamu


Na Mwandishi Wetu
Mchungaji wa Kanisa la Hosana Msigani Linalotambulika kama Ngome ya Yesu Mzola amewashanga wengi kutokana na nguvu za uponyaji anazozifanya pamoja na kuwasambaratisha wachawi.
Mtandao huu wa maskanibongotz ulifika kwenye Kanisa hilo kujionea namna ya ibada zake zinavyofanyika baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa nguvu za ajabu za mchungaji huyo sio za kawaida kutokana na uponyaji wake anaoufanya wa papo kwa hapo.
Akiongea na mtandao huu mchungaji huyo alisema" Mtumishi haya unayoyaona hapa ni nguvu za mungu wa kweli na sio maigizo kwani Mungu wa hapa sio wa masihara wala utani hivyo ukija mgonjwa dozi utakayoipata hapa  basi unakuwa mzima milele iliamradi usitende dhambi tena" Alisema Mchungaji huyo na kutoa namba yake ya simu kwa mtu yeyote anaehitaji maombezi kwa njia ya simu 0713-161785 na watu watapokea mujiza hapo walipo.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king