Sadick Hamid mkurugenzi wa SADICKTV sehemu ya mapokezi kwenye kituo cha E-fm Radio
Sadick Hamid akiwa na mzee Kitime ndani ya studio za kisasa ndani ya E-fm Radio |
Sadick Hamid kushoto akisalimia na mwenyeji wake Livingstone Mkoi ambae ndiye mkuu wa kitengo cha habari ngumu za uchunguzi
Ripota wa Sadicktv kwa Mkoa wa Dar es Salaam nae alifurahi kutembelea studio hizo
Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi, Mwandishi na mfanyabishara maarufu Mkoani Tanga
ambae ni kijana mdogo Sadick Hamid ambae ni mkurugenzi wa kituo cha “SADICKTV”
siku ya jana amefanya ziara kwenye kituo bora cha matangazo ya E-FM Radio 93.7
na kupokelewe na mkuu wa kitengo cha habari za Uchunguzi ndani ya E-fm Radio Bw
Livingstone Mkoi.
Mkurugenzi huyo akiambatana na maofisa wake walifika kwenye
radio hiyo jana saa mbili usiku na kufanya mazungumzo mafupi na Bw Livingstone
Mkoi ambapo Sadick alianza kuupongeza uongozi wa kituo hicho kwa kuwa na
mitambo ya kisasa” Kaka kiukweli nimetembea kwenye vituo vingi sana hapa Afrika
lakini kwa hii mitambo yenu nimeikuta South Afrika tu “ Alisema Mkurugenzi huyo
Aidha mkurugenzi huyo
ambae kwa utafiti usiokuwa rasmi umemthibitisha kuwa mfanyabishara mwenye
umri mdogo kuwa na pesa ndefu Mkoa wa Tanga, alisema kufanya
ziara hiyo ndani ya kituo hicho kimemfundisha mengi na kumpa wivu wa maendeleo
zaidi ili kulipeleka taifa mbele kwa maendeleo ya haki na kweli.
Akiwa ndani ya kituo hicho alikutana na mwanamuziki Mkongwe
Mzee Kitime
0 comments:
Post a Comment