Mchungaji
Andrew White wa kanisa Anglikana Baghdad.
|
Kundi hatari linalodai kutetea haki
za waislamu la ISIS la nchini Iraq limewachinja watoto wapatao wanne wenye umri
chini ya miaka 15 baada ya watoto hao kukataa kumkana Yesu na kumfuata mtume
Muhammad kama walivyotakiwa na wapiganaji wa kundi hilo.
Kwa mujibu taarifa zilizonaswa na maskanibongotz za mchungaji kiongozi wa kanisa
Anglikana Baghdad canon Andrew White aliweka wazi tukio hilo alipohojiwa hivi
karibuni na CBN na kutolewa kwenye mtandao wa Orthodox Christian Network,
amesema ISIS waliwakamata watoto hao wanne na kuwaambia wafuatishe maneno
watakayowaambia ya kumfuata Muhammad, lakini watoto hao kwa pamoja wakasema
hapana …"siku zote tumekuwa tukimfuata Yasua (Yesu), Yasua amekuwa pamoja nasi
siku zote" walisema watoto hao kama ilivyowekwa wazi na mchungaji White
Wapiganaji hao wakaendelea kuwataka watoto hao kubadili msimamo wao kwa
kufuatisha maneno
yao lakini watoto hao wakaonyesha
msimamo wa kukataa amri ya wapiganaji hao kitendo ambacho wapiganaji hao
wakatoa visu vyao na kuwachinja watoto hao. "Utafanyaje katika hali kama
hiyo? mchungaji White aliuliza,"utabaki unalia, wote ni watoto wangu, hayo
ndiyo tumekuwa tukiyapitia alisema mchungaji White ambaye amebaki pekee kitendo
kilichosababisha kupewa uongozi wa Baghdad kwa kanisa hilo.
Aidha katika tukio lingine
lililowekwa wazi na mchungaji White ambaye kwasasa yupo nchini Israeli baada ya
kutishiwa maisha yake na wapiganaji wa ISIS, amesema baada ya tukio la watoto
hao, mwanaume mwingine jijini Baghdad aliwekwa chini ya ulinzi na wapiganaji wa
ISIS waliomtaka kusema maneno ya kuukataa Ukristo na kumfuata Muhammad lasivyo
watachinja watoto wake kitendo kilichosababisha mwanaume huyo kusema maneno ya
wapiganaji hao, kisha baade kumpigia simu mchungaji White akiuliza kama Yesu
bado anampenda kwakuwa siku zote amekuwa akimpenda Yesu je kwakufutisha maneno
ya ISIS inamaana Yesu hampendi tena, kwani alisema hivyo tu ili kuzuia kuona
watoto wake wakichinjwa, ambapo mchungaji White akamjibu baba huyo kwamba Yesu
bado anampenda.
Creedit:maskanibongotz
|
0 comments:
Post a Comment