Tuesday, November 17, 2015

DC MAKONDA NI MTU HATARI SANA KULIKO WACHACHE WANAVYOMCHUKULIA, ANGALIA HAPA ALIVYOZIMA JARIBIO LA HATARI KWENYE KIWANDA CHA URAFIKI, WAKAZI JIJINI WAZIDI KUMUOMBA RAIS MAGUFULI KUHUSU MKUU HUYU WA WILAYA, ANGALIA HAPA ALICHOKIFANYA..!

Wiki iliyopita wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha urafiki walifanya mgomo kwa madai ya kutolipwa mishahara yao kwa muda mrefu
Leo mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda alikutana na wafanyakazi wa kiwanda hicho, Dar es salaam na kufanya mazungumzo nao ikiwa kusikiliza kero zao, kisha kufikia muafaka wa wao kurudi kazini na kuendelea na shughuli kama kawaida.
Amesema atakutana na Rais Dk. John Magufuli ili kuweza kumweleza matatizo ya wananchi wa Wilaya yake na kulitafutia ufumbuzi.
“Nimevunja ratiba zote ili nije kuwasikiliza, nataka kutoa kikomo changu kuanzia tarehe 1 mwezi ujao wakati tunakwenda kula sikukuu za Krismas na mwaka mpya kila mtu awe amelipwa mafao yake, agizo langu la kwanza kwa uongozi kesho wakutane kwenye mahakama husika pamoja na viongozi wenu wa watumishi kwa ajili ya kupitia malipo yenu ili yaweze kufanana”… Paul Makonda.
“Nyinyi mtakaporidhika wao waonyeshe utekelezaji umefikia wapi, kitakachokwenda kufanyika kwenye mahakama ni kuoanisha kuwa mnastahili kulipwa? unaweza kukuta umeandikiwa unatakiwa kulipwa elfu 80, iyo elfu 70 inakwenda wapi, lazima mfahamu?..Makonda
Kingine Makonda amewataka viongozi wa kiwanda hicho “ifikapo tarehe 24 mwezi huu uongozi utakapomaliza maamuzi ubandike matangazo jinsi mtakavyolipwa pesa zenu na baada ya kuwa mmelipwa ziko taratibu za kisheria juu ya nani mwenye sifa ya kuwa mwajiriwa wa kudumu, katiba nyingine inatoa mamlaka kwa wafanyakazi, mlilolifanya ni tendo la kikatiba, ni haki yenu ya msingi” Makonda.
Makonda amewaomba wafanyakazi wote waweze kurudi kazini kuendelea na kazi kama kawaida.
DSC_9541
Paul Makonda akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha Urafiki, Hata hivyo wananchi mbalimbali Jijini Dar wameendelea kumuomba Rais Mgufuli kumpandisha sheo Mh Paul Makonda kutokana na utendaji wake mzuri ambapo kwa sasa Wilaya zote  Jijini Dar zinatamani awe kiongozi wao kutokana na kuweza kutatua migogoro ya wananchi kwa wakati.
Credit: maskanibongotz

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king