Tuesday, October 21, 2014

BREAKING NEWS: KIGOGO SUGU WA MADAWA YA KULEVYA ADAIWA KUKAMATWA KIMAFIA JIJINI DAR. AKUTWA NA MIFUKO KIBAO. WANANCHI MAGOMENI WAMUANDALIA ZAWADI KAMANDA NZOWA...!


 KAMANDA WA KIKOSI MAALUM CHA KUPAMBANA MADAWA YA KULEVYA NCHINI NZOWA
 KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM JIJINI DAR BWA SULEIMAN KOVA
KAMANDA WA POLISI KANDA YA KINONDONI WAMBURA
Na Mwandishi Maalum
Habari zilizonaswa na mtandao huu leo mapema zinasema kuwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum kushirikiana na Usalama wa Taifa limemkamata kigogo aliyekuwa tishio wa madawa ya kulevya "Jina linahifadhiwa kwanza" pamoja na wapambe wake watano maeneo ya Magomeni Jijini Dar.
Habari toka kwa chanzo chetu cha habari toka kituo cha Polisi Oysterbay ambae aliomba hifadhi ya jina lake kwa maana yeye si msemaji alisema kuwa kibopa huyo maarufu sana na alikuwa hakamatiki kirahisi lakini hatimae amekamatwa  na ushahidi ubaoni kimafia na wanausalama hao na kupelekewa sehemu siyojulikana kwa ajili ya mahojiano.
Habari zaidi zilieleza kuwa tajiri huyo ambae alikuwa akiwasumbua vichwa Polisi namna ya kumkamata kwa kukosa ushahidi lakini hatimae usiku wa kumakia Jumanne saa nane usiku kundi la wana usalama lilivamia na kumkamata kimafia huku risasi zikilindima ambapo alikuwa akichanganya mzigo huo ambao haujajulikana thamani yake.
Hata hivyo mtandao huu ulifanya jitihada za kuwasiliana na Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni Camilius Wambura ili kuzungumzia tukio hilo hakuweza kupatikana baada ya simu yake kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Aidha mtandao huu unafanyajitihada za kumtafuta Kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Bw Suleimani Kova ili azungumzie tukio hilo.
Hata hivyo wakazi wa Magomeni wameuambia mtandao huu kuwa waamemuandalia zwadi nono ya kumpongeza Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini Nzowa kama kweli hizi taarifa za kumatwa kwa mtu aliyewatesa watoto wao miaka mingi kwa madawa ya kulevya.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king