KWELI SIFA ZIKIZIDI SANA MWISHO MAJANGA...!
Na Mwandishi Wetu
Ukisikia yanazungumzwa maskani huko utadhani kama ni masihara lakini huo ndiyo ukweli kwamba mwanamuziki Diamond amekalia kuti kavu kufuatia kutafutwa vibaya na Jeshi la Polisi Kanda ya Kinondoni pamoja na Ma-Mp wa JWTZ kwa ajili ya kueleza alikozipata sale zao ama kuonesha mtambo wa kutengezea hizo sale.
Habari za uhakika zilizonaswa na mtandao huu zilisema kuwa tayari hadi sasa Wacheza shoo wa mwanamuziki huyo wamekamatwa wapo ndani ya nondo kituo cha Polisi Oysterbay pamoja na Meneja wake Babu Tale.
Licha watu kwa sasa wananyea debe bila kujua hatima yake Diamond mwenyewe amejificha na wala hajulikani alipo huku simu zake hazipatikani hata nyumbani kwake hayupo na tayari imedaiwa maofisa hao wa Polisi kushirikiana na wale wa Jwtz wamingia mtaani kumsaka na kuna zawaidi nono itatolewa kwa atakaefanikisha kukamatwa kwake muda wowote.
Hata hivyo kwa mujibu wa mtu mmoja ambae ni Askari pale Oysterbay Polisi alisema kuwa mwanamuziki huyo atakapokamatwa huenda akapelewa Mkoani Morogoro pamoja wenzake kambini
Hata hivyo kwa mujibu wa mtu mmoja ambae ni Askari pale Oysterbay Polisi alisema kuwa mwanamuziki huyo atakapokamatwa huenda akapelewa Mkoani Morogoro pamoja wenzake kambini
Credit: Maskanibongotz
0 comments:
Post a Comment