Monday, October 20, 2014

ZALI LA MENTALI: MAAFANDE WALIOFUKUZWA KAZI KWA MAHABA WAPATA TENDA YA KUCHEZA FILAMU. WAANDALIWA MAPOKEZI MAKUBWA JIJINI DAR. MANAIKI SANGA ARATIBU UJIO WAO...!

 VERONICA MDEME AKIWA KWENYE PICHA YA POZI
 VERONICA NA AFANDE MWENZAKE WAKIWA KWENYE MAHABA MAZITO

MTAALAMU MWENYEWE: MANAIKI SANGA THE DON AKIWA NA MWANAMUZIKI WA BONGO FLAVA TOKA ZANZIBAR MAARUFU KWA JINA LA DIDA AMBAE NI MTOTO WA MJANE WA MWISHO  WA RAIS WA KWANZA WA ZANIBAR MZEE KARUME

IRENE UWOYA NA MANAIKI SANGA.
Na Sakina Shabani
Kweli ustaa hauji bila skendo hivi ndivyo zali la mentali lilivyowafikia maafande wawili waliofukuzwa kazi hivi karibuni kwa kuonesha mahaba hadharani tena wakiwa kwenye sale za kazi kinyume na utaratibu wa kazi ya upolisi. Maskanibongotz linakupa mkanda mzima.

Taarifa za uhakika zilizonaswa na mtandao huu hatari kwa umbea zilisema kuwa maafande hao huenda sasa wakaondokana na umasikini kutokana na kupata nafasi ya kucheza filamu na kampuni ya MK PRODUCTION inayomilikiwa na msanii aliyejizolea umaarufu nchini na Dunia kwa picha za ngono Manaiki Sanga.

Chanzo hicho makini kiliendelea kuuleza mtandao huu kuwa Maafande hao wataingia mkataba wa miaka mitano ya kucheza filamu na watapewa seen za mahaba kutokana na kipaji walichokionesha kwenye picha hiyo iliyowafukuzisha kazi.
Mtandao huu ulifanya jitihada za kumtafuta msanii Manaiki Sanga ili kueleza ukweli wa taarifa hizo na alipatikana kufunguka hivi " Ni kweli kamapuni yangu imekwishafanya mazungumzo ya awali kwa ajili ya kuingia mkataba na maafande hao na tayari Director wangu kesha waandalia cript zao nasubiri waje tu Dar kisha waingie mzigoni" Alisema

Hata hivyo Manaiki aliongeza kusema" Nimeguswa sana na tukio la kufukuzwa kazi maafande hao na nimeona wana vipaji wakiwezeshwa wanaweza kujiingizia kipato kikubwa na wameonesha wavipaji sana hasa wakipewa seen za mapenzi watafanya vizuri ikizingatia umri wao bado mdogo hivyo watanzania wenzangu tuwape sapoti" Alimaliza kusema

Maskanibongotz bado unaendelea kuwatafuta maafande hao ili kuzungumzia ishu hiyo ya kuamua kujiingiza kwenye filamu ili kukuza vipaji vyao na tunawaahidi next time tutawaleta mazungumzo yao
CREDIT: MASKANIBONGOTZ

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king