Wakurugenzi wa Clouds Media. kushoto ni MD, Joseph Kusaga "Brother Jo" na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Luge Muhahaba
Hii ndiyo barua iliyotolewa na Mahakama ikiwataka Clouds Fm na Prime Promotion wasimpandishe Davido kwenye shoo ya Fiesta kwa vile tayari ana mkataba na kituo cha Radio Times 100.5 lakini Clouds Media ilimpandisha kinguvu bila kutii amri hiyo ya mahakama.
Hata hivyo tukio hilo limevuta hisia tofauti kwa wakazi wa Jiji la Dar huku wengi wao wakitoa maoni kwa uongozi wa kituo cha Clouds Fm kuwa ifikie mahara waachane na bifu zisizo na msingi kwa vile katika maisha ni heri kupunguza maadui kuliko kila kukicha unaongeza maadui.
Akiongea kwa shart la kutotaja jina lake meneja wa televishisheni moja iliyopa ukanda wa Ziwa alisema" Kiukweli mimi namshauri kakaangu mpendwa Joseph Kusaga kufika wakati kuachana na marumbano yasiyo na tija yeye ni mmoja wa wafanyabishara wenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi hii hivyo jamii inavyoona haya yanatokea wanajifunza nini" Alisema meneja huyo wa radio na tv
Aidha meneja huyo aliongeza kusema kuwa anajaribu kuangalia mbali kwa mahusiano yatakuaje kwani leo hii wamewafanyia Times je unadhani kutakuwa na amani tena kati ya media hizo? Jibu hapana hivyo ni vyema kuacha kuingia bifu na watu kila akukicha ni jambo hatari sana katika maisha ya kibiashara hata kwa Mungu haipendezi laana yake huwa ni mbaya sana na itasambaa vizazi kwa vizazi.
0 comments:
Post a Comment