Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli, wananchi wa Kinondoni wanamuomba asimuondoe Makonda kwenye Wilaya hiyo kwa vile bado wanahitaji msaada wake wa kutumbua majibu ya Ardhi kwenye Mansptaa ya Kinondoni.
DC Makonda akiwa kwenye majukumu yake |
Hapa ni wananchi wa Nyakasangwe kata ya Wazo wakiwa na mabango ya kuwakataa maafisa Ardhi Kinondoni ambao wamekuwa tishio wa ufisadi wa ardhi kwa kushirikiana na matajiri wakubwa.
Na Mwandishi Wetu
Wilaya ya Kinondoni yenye wakazi wengi pengine kuliko Wilaya zote nchini Tanzania huku Wilaya hiyo ikiwa na changamoto rukuki za maendeleo, huku vijana wengi wakiwa hawana ajira, migogoro ya Ardhi nayo pia ikiwa tishio licha ya kwamba ni Wilaya ambayo ipo Jijini Dar mjini.
Kufuatia kuwepo kwa taarifa za ubadilishwaji wa wakuu wa Wilaya huku wengine ikidaiwa kupumnzishwa kabisa, hii inatokana masimamo wa Mh Rais John Pombe Mgufuli kutaka kupata watendaji kazi wazuri na sio mizigo kama ilivyokuwa kwa Serikali iliyopita, hivyo wananchi hao wamemuomba Rais kwenye panga pangua hiyo awaachie Mh Paul Makonda kwani tayari ameshafanikiwa kuiweka sawa Wilaya ya Kinondoni.
Wakiongea na Maskanibongotv pamoja na mtandao wa kijamii wa maskanibongotz wananchi hao walisema “ Ndugu Mwandishi kweli tunamuomba Rais Wetu John Pombe Magufuli atuachie Mkuu wetu wa Wilaya Mheshiwa Makonda kiukweli tayari amekuwa tegemeo kwetu sisi wananchi wanyonge na hata vijana wetu wapo kwenye mipango mzuri ya ajira ambayo Makonda amekwishaipanga” Walisema watu hao.
Hata hivyo mmoja wa wananchi wa kata ya Wazo mtaa wa Nyakasangwe Manaiki Sanga ambae ni muhanga wa Mgogoro wa Ardhi alisema” Tuna imani na Mheshimwa Rais Magufuli ambae ni tofauti na viongozi waliopita tunaamini kwenye maamuzi yake atatumia busara kumuacha Makonda kwenye Wilayah ii kwa vile hadi sasa ameokoa maisha ya watu kwa kupambana na ufisadi wa ardhi ambapo mwaka juzi ulipoteza maisha ya wananchi, lakini kwa sasa hali ya ulinzi na usalama umeimalika kutokana na hujudi zake” Alisema
DC MAKONDA ni mkuu wa Wilaya mtenda haki mtetezi wa wanyonge ambae matajiri wengi na mafisadi ndiyo adui zake kwa maana wanamchukia kwa msimamo wake kwenye kazi, pia wanasiasa wamekuwa na kinyongo nae kutokana na chuki zao binafsi, lakini kiukweli Makonda amekuwa mmoja wa wakuu wa wilaya wachache wanaofanyakazi zao bila uwoga na kujituma kiasi kwamba hata Wilaya nyingine zimekuwa zikimuhitaji ili akaweke mambo sawa.
Kwa kilio hichi cha wananchi tunaamini Mheshimiwa Rais wa John Pombe Magufuli atasikia na kumbakisha DC Makonda ili aendelee kuwatetea wanyonge na kupambana na mafisadi.
Credit: Maskanibongotz
0 comments:
Post a Comment