Na Mwandishi wa Maskanibongotz
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda amevunja rekodi ya kipekee kwa
kuanza kutekeleza ahadi aliyoitoa Mh Rais Magufuli kwenye hotuba yake
aliyoitoa mwishoni mwa wiki iliyopita ya kuanza harakati za kuwapimia
wananchi ardhi zao na kuwapatia hati miliki zao.
Makonda
ambae wengi hupenda kumuita Nabii kutokana na kila atakalolizungumza
kwa wakati ujao na huwa hivyo hivyo alivyozungumza, ambapo Mkuu huyo
aliwahi kumtabiria Umakamo wa Rais Mhe.Samia
Suluhu mwaka mmoja baadae hali hiyo ikaja kutokea kweli, na wiki
iliyopita kabla Mh Rais hajahutubia Bunge na kuanisha mambo muhimu
atakayoanza kuyashughurikia, Dc Makonda alizungumza na na Wana habari
kuhusu kuanza zoezi la kuhakiki viwanja vyote vyenye Migogoro kisha
kuvipatia ufumbuzi.
Kauri
hiyo pia ikaja kudhihirishwa na Mh Rais ya kuhakikisha wananchi wote
wanapimiwa ardhi zao na kupewa hati miliki, wiki hii ofisi ya Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni itatoa ratiba ya kuanza kwa zoezi hilo la kuhakiki
viwanja hivyo harafu hatua ya kuimwa ianze kwa kata tatu za Bunje,
Madale, na Wazo ambalo maeneo ya Nakasangwe na Nakalekwa ndiye yenye
shida sana kutokana na mafisaidi kutumia nguvu ya pesa kuwanyanyasa
wakazi hao wanyonge.
Kufuatia
hatua hiyo wakazi hao ambao wamesema wana imani na Dc huyo na wanaamini
mafisadi hawawezi kumuhonga kama walivyo mtuhumu DC aliyemtangulia Jordan Lugimbana ambae wakazi hao wanadai mafisadi walimshika kisawa sawa na kushindwa kufurukuta kwa nguvu ya pesa.
Hata
hivyo wakazi wa Nakasangwe na Nakalekwa toka wiki iliyopita wako kwenye
maombi maalum ya kumuomba Mungu amuonngoze vyema Dc huyo kwani ndiye
pekee wanaemtegemea kwa sasa kwani katika maafisa wake wa Ardhi nao
hawana imani nao kutokana na kuwepo kwenye mkumbo wa rushwa za mafisadi
hao .
Wakiongea
na maskanibongotz wakazi hao ambao ni watu wazee na vijina wakina mama
na wakina baba walisema" Ndugu mwandishi sisi tunaweza kusema kuwa kwa
sasa roho na matumaini yetu yako kwa Dc Makonda tu tunamuombea kwa Mungu
amuongoze atende haki kwa kusimamia mwenyewe zoezi hili kwani maafisa
ardhi wake tulishakosa imani nao siku nyingi kipindi cha Jordan Lugimbana , hivyo watanzania wapenda haki tuungane kumuombea Dc huyo" Walisema wananchi hao.
Kwa
kumalizia kumuomba Dc kwenye utekelezaji wa zoezi hilo watu wote wenye
vibanda vyao tayari na wanaishi wapewe kipaumbele na hayo maeneo mengine
ya ambayo watu hawajajenga ndiyo wapewe hao mafisadi.
Mtandao
huu bado unaendelea kumtafuta Dc Makonda ili azungumzie zoezi hilo
litaanza tarehe ngapi rasim na wataanza kata gani kati ya hizo
zilizotajwa hapo juu, na tutawaleta majibu mapoema iwezekanavyo.
Credit: Maskanibongotz
0 comments:
Post a Comment