Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli, ambae anasubiriwa kwa hamu na wakazi wa Kata
ya Wazo na
Nakasangwe au "Kaza Roho" wanaimani atamaliza mgogoro wao wa ardhi ambao
una harufu ya rushwa toka wawekezaji na baadhi ya watumishi wa Manispaa
ya Kinondoni na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao
wanalalamikiwa na wananchi kwa uonevu wanaofanyiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiq.
Credit: maskanibongotz
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiq.
Mkuu
wa Wiyala ya Kinondoni Paul Makonda aliyevaa miwani akiwa amekaa chini akiwa na wakazi hao wa Nakasangwe kata ya Wazo
akiwasikiliza malalamiko yao juu ya mafisadi hao, na Dc huyo kugundua
wazi kuwa kuna uonevu mkubwa kwa wakazi hao.
Wamtaka
afike kuona nguvu ya ufisadi inavyofanya kazi huku baadhi ya watumishi
wa Manispaa ya Kinondoni wakihusishwa. DC Makonda Apongezwa.
RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AOMBWA KUFIKA KATA YA WAZO NA NKASANGWE KUJIONEA NGUVU YA UFISADI WA ARDHI, WANANCHI WAMUANDALIA MAPOKEZI MAKUBWA. DC PAUL MAKONDA ATOA ANGALIZO ASEMA ISHU HIYO HUENDA INA KIGOGO MZITO WA SERIKALI MWENYE CHEO KULIKO YEYE ..!
Na Mwandishi Wetu
Wakazi
wa Kata ya Wazo na
Nakasangwe wamemuomba Rais Dokta John Pombe Magufuli kuanza ziara kwenye
kata hiyo ili kushuhudia uonevu na ubabe unaofanywa na watu wanaojiita
wawekezaji kwa kuwavunjia watu makazi yao huku wakidai kuwa ni yao.
Wakazi
hao ambao wamesheherekea zaidi ya siku 3 ushindi wa Rais huyo ambae
wanamini ataweza kuwasaidia na kuwasambaratisha mafisadi hao ambao wana
nguvu ya ajabu kutokana na kuwa na pesa nyingi ambazo ilidaiwa waliweza
kuhonga baadhi ya watumishi wa Mkoa pamoja na Manispaa ili wawezeshe
kuwavunjia nyumba zao na kuwahamisha na zoezi hilo lililofanikiwa.
Katika kikao kilichofanyika hivi karibuni cha Mkuu
wa Wilaya aliandamana na Mkurugenzi wa Manspaa ya Kinondoni, Afisa
Ardhi wa Manspaa na maofisa wengine toka Wilayani akiwepo RPC Wambura na
kwa kauri yake Mkuu wa Wilaya hiyo na wakazi walioathirika na ubabe huo
wa wawekezaji, Dc huyo aligundua chanzo cha mgogoro huo kuwa ni rushwa
na si kitu kingine na kuahidi kupambana kwa kadri atakavyoweza ili
wananchi hao wapate haki yao ya makazi.
Hata
hivyo Mkuu huyo wa Wilaya alitoa angalizo kuwa mgogoro huo huenda nyuma
yake kuna mtu mwenye nguvu kuliko yeye hivyo ni heri pia wananchi
hao wakashirikiana na Mwenyekiti wao wa mtaa ili wapate timu itakayokuwa
inasimamia ufatiliaji.
Wakiongea
na gazeti hili wakazi wa eneo hilo ambao waliothiriwa na ubabe wa
mafisaidi hao mmoja wa wakazi hao ambae ni mwandishi wa kituo cha E-fm
Radio Bwana Livingstone Mkoi alisema" Kiukweli hali haikuwa nzuri tangu
2012-13 wananchi wengi tulipoteza mali zetu, makazi yetu mengi yavunjwa
kibabe na Polisi waliodai kutumwa na Mkuu wa Wilaya aliyepita Mh Jordan
Rugimbana kwa madai kuwa sisi tumevamia eneo la mwekezaji na kuongeza kuwa sisi si raia wa Tanzania , na kila
tulipoenda ofisini kwake kwa ajiri kufanya mazungumzo ya amani na
kumueleza kama eneo hilo sisi tulipewa na Serikali kupitia Mkuu wa Mkoa
Mh Yusuph Makamba, alitoa majibu kuwa huo utekelezaji ni maagizo toka
ofisi ya Mkuu wa Mkoa" Alisema Mwandishi huyo
Mwandishi
huyo aliongeza kusema kutokana na nguvu fedha utekelezaji wa kubomoa
nyumba hizo ulitimizwa chini ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kwa
ubabe mkubwa, lakini hata hivyo suala hilo lilitinga kwenye chombo cha
Sheria na hatimae wakazi hao walishinda kesi na Manispaa kuamuriwa
kuwalipa fidia wakazi hao kwa vile walikuwa wakiishi kihalali eneo hilo
kwa vile upande wa team mafisadi ulishindwa kuwakilisha vielelezo vya
msingi vinavyoonesha kuwa hilo ni eneo lao, hata hivyo katika hali
nyingine mafisadi hao walifungua tena kesi nyingine ambayo inaendelea
hadi sasa.
Hata
hivyo wakazi hao wanaimani na Rais Dokta John Pombe Magufuli atasaidia
kusambaratisha mtandao huo wa ufisadi ambao unaodaiwa kuanzaia ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Maofisa Ardhi wa Manispaa ya Kinodoni
ili wananchi hao
waishi kama watanzania halisi na kuondoa dhana kwamba wao ni wavamizi na
sio raia wa Tanzania ndio kesi waliyopewa, huku tuhuma hizo zikiletwa
kwenye kipindi kisichokuwa cha uchaguzi lakini kipindi cha uchaguzi
madai hayo huwa hayapo.Credit: maskanibongotz
0 comments:
Post a Comment