Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar -es Salaam Bwana Suleiman Kova. Ambae ameombwa kuwasidia wanawake hao wanyonge ili watuhumiwa wao waweze kupatikana na kufikisha mahakamani au kuwalipa pesa zao walizopigwa kwa njia ya utapeli
Brigitte Vitalis na husband wake Norberth Edward Hizza ambao wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Brigitte Vitalis na husband wake Norberth Edward Hizza .
Brigitte Vitalis na husband wake Norberth Edward Hizza .
Brigitte Vitalis na husband wake Norberth Edward Hizza wakifurahia maisha baada ya kudaiwa kutoka kumpiga dada huyo wa kiarabu milioni tisa kwa kuchukua vitu mbalimbali vyenye samani hiyo.
Bingwa Brigitte Vitalis akiongea na simu kwa ajiri ya mipango ya kazi huku mumewe Norberth Edward Hizza akisikiliza mchongo.
Na Sakina Shabani
Surutana Khamis ambae ni mmoja wa wahanga waliojitokeza kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu kudaiwa kutapeliwa na wananandoa hawa Brigitte Vitalis na mumewe aitwae Norberth Edward Hizza milioni tisa baada ya kuchukua vitu vya gharama hizo dukani kwake.
Akizungumza juzi na gazeti hili Surutana Khamis amesema atadai haki yake hadi tone la mwisho na hata kama mkono wa dola ukishindwa kuwanasa watu hao ili wamrudishie mali zake basi atatumia njia mbadala ambayo ni dua maalum ili kwani kamwe jasho lake haliwezi kwenda bure.
Akizungumza juzi pia na wana habari juzi Surutana amesikitishwa na kauri anazotoa Norberth Edward Hizza kuwa eti yeye hausiki kwenye hizi kesi za utapeli" Huyu kaka kwenye hii kesi MARB97682015 KUJIPATIA MALI KWA NJIA YA UDANGANYIFU yeye ni mtuhumiwa namba moja kwa vile ndiye aliyekuja kuchukua vitu dukani, hivyo asitake kujisafisha mtaani huko alikojificha aende pale Polisi kwa Mkuu wa Upelelezi, au OCD wa Magomeni akiwa na RB hiyo kisha alalamike kwamba yeye hausiki na kachafuliwa halfu majibu yake atayapata pale" Alisema msichana huyo kwa uchungu kutokana na kwa sasa kuyumba kibiashara kutokana pesa yote kumalizikia kwa Brigitte Vitalis na Norberth Edward Hizza.
Surutana Khamis aliongeza kusema kuwa kama Norberth anaona kweli yeye anasingiziwa basi anende hata kwa Kamanda Kova na hiyo RB aseme ni ya uongo ili sisi tushtakiwe kwa kugushi taarifa hiyo na kundi nzima kati yetu tushtakiwe.
Dada huyo aliendelea kusema kuwa yeye ni mmoja kati ya wanawake wanaojitafutia ridhiki kwa haki hivyo ni vyema hata Serikali kupitia Jeshi la Polisi wawasaidie kukamatwa kwa watuhumiwa hao kwa vile wanawake wanaodaiwa kutapeliwa wapo wengi, hata tangu habari hizi zianze kusambaa mitandaoni na magazetini watu wengi zaidi wamejitokeza nao wakilalamika kutapeliwa na Brigitte Vitalis lakini huku wakisubiri kama atakamatwa basi wajazane Polisi kwani wengi wamemtafuta bila mafanikio.
Hata hivyo Surutana kushirikiana na wale wanawake wengine wanyonge wenye kesi namba hii OB/RB/11345/2014 JALADA LA UCHUNGUZI ya mwaka jana, na nyingine ya mwandishi wa habari aitwae Teddy Dinghoka milioni kumi na mbali. ambae alipigwa milioni kumi na mbili wote kwa pamoja wameshukuru Jeshi la Polisi Kanda ya Kinondoni kwani hadi sasa wanaendelea kufanya msako mkali wa nyumba hadi nyumba na Mungu mkubwa huenda siku si nyingi watuhumiwa hao watadakwa na kufikishwa mbele ya pilato kwa tuhuma hizo nzito.
Hata hivyo walitafutwa wanandoa hao kwa njia ya simu ambao simu zao ziliita tu bila majibu na kuna taarifa kama namba ngeni hawawezi kupokea kutokana na hofu ya kukamatwa na Polisi.
0 comments:
Post a Comment