Mh Paul Makonda . maskanibongotz |
Hii ndiyo shughuri aliyokutana nayo Makonda jana huko Nakalekwa maskanibongotz
Hapa DC huyo akiwaombea msamaha kwa kuhiswa vibaya watumishi hao na kuwahisi watu wamesiwe na shakana kuhusu zoezi hilo kuwa litakwenda vizuri kwa baraka za Mungu. maskanibongotz
Na Mwandishi wa maskanibongotz
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua, Hali ya usalama
ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda kwa sasa huenda ikawa
mashakani baada ya kujitoa muhanga kupambana na ufisadi mkubwa unaofanywa na
matajiri wenye mgogoro wa ardhi na wananchi wanyonge kwenye Kata ya Wazo mtaa
wa Nyakasangwe na Nakalekwa, huku nyuma ya matajiri hao kuna vigogo wakubwa wa
Serikali wenye nguvu kuliko yeye.
Habari za uhakika toka kwa vyanzo vyetu makini ambavyo havina
hata chembe ya shaka viliuleza mtandao huu wa maskanibongotz kuwa Mkuu huyo wa
Wilaya ambae amekuwa mstari wa mbele kutetea wanyonge hasa wanaoonewa kwenye
masuala haya ya ardhi lakini mtihani mkubwa uliopo ni nguvu ya pesa kwani
mafisadi wamewakamata watu wa mipango miji Manspaa ya Kinondoni, Watu wa Ardhi
na hata msaidizi wa Dc huyo.
Mkuu huyo wa Wilaya wiki hii tarehe 25 mwezi huu ilikuwa ufanye
mkutano na wakazi hao wa Nakasangwe na Nakalekwa ilikuwa kwa ajiri ya kuwaeleza
wakazi hao namna alivyofanya jitihada za ziada kufanya vikao na pande zote
mbili yani viongozi wa Serikali ya mtaa huo akiwa na kamati iliyokuwa
imeteuliwa kwa ajiri ya kusimamia vikao
vya usuruhishi lakini pia timu ya pili ni ile ya watu wanaodai kuwa maeneo hayo
wanayoishi wananchi ni yao.
Hata hivyo vikwazo vilianza kuingia baada ya Mkuu huyo wa
Wilaya kufika kwa muda mrefu huku akiwasubiri maafisa Ardhi ambao walidaiwa
walikuwa wametokea kwenye kikao cha siri na mafisadi hao kwa lengo la
kukwamisha zoei hilo lisiende sawa kama lilivyokuwa limepangwa ambapo baadae
walipofika maafisa hao kumi na moja Dc huyo aliamuru kuwaweka ndani kwa uzembe
walioufanya lakini si hivyo inadaiwa mkuu huyo wa Wilaya nae alikuwa amepata
taarifa za wapi walipokuwa wamepitia.
Kwa siku hiyo ya tarehe 25 zoezi hilo lilikwamba ambapo Mkuu
wa Wilaya alimuagiza Mwenyekiti wa Nakasangwe Peter awaombe radhi wananchi kwa
niaba yake kwa tukio lililokuwa limetokea na kuahidi zoezi hilo kuendelea kesho
yake ambayo ni jana tarehe 26.
Hata hivyo siku hiyo ya jana wakazi hao zaidi ya elfu 30
walikusanyika mapema sana kwa ajiri ya kumsubiri Mkuu huyo wa Wilaya ili
wamsikilize ambapo mapema tu kiongozi huyo anaechukia rushwa alifika akiwa
ameongozana na wale maafisa Ardhi na watu wa mpango miji, Rpc Wambura na wale
watu wa upande wa pili wanaodai maeneo hayo ni yao.
Baada ya kufika eneo la uwanja wa CCM Nakalekwa Mkuu
huyowa wilaya alikutana na mabango yenye jumbe za kushtua ambapo mabango hayo
yaliyokuwa yanasema kuwa wakazi hao hawana imani na watu wa mipango miji kwa
vile kuna taarifa wanashirikiana na
mafisaidi, huku pia wakazi hao wakimkataa moja kwa moja DASI msaidizi wa
Mkuu wa Wilaya kwa madai kuwa yumo kwenye mtandao wa kushirikiana na mafisadi hao ili wawadhurumu
wakazi hao ardhi yao.
Sehemu hiyo ya mabango pia ili muomba Rais Dokta John Pombe
Magufuli kuwashughurikia watu wa Mipando Miji na maafisa Ardhi kwa madai ya ufisadi na
mambo mengine mabango hayo kama yanvoonekana pichani, hata hivyo hali hiyo
ilimshtua Mkuu huyo wa Wilaya na kuwasihi wakazi hao kuwaamini maafisa ardhi
wake kwani nay eye atakuwepo kwenye zoezi kwa siku za awari jambo ambalo
lilipingwa vikali na wakazi hao kwa kuonesha wasi wasi wao kuwa endapo
wakiachiwa maafisa ardhi hao peke yao bila yeye Dc huenda zoezi hilo lingeleta
utata na ndichp kilichotokea leo tarhe 27.
Zoezi hilo kwa jana alilienda swa kwa vile Mkuu wa Wilaya
alilisimamia vizuri lakini siku ya leo tarehe 27 zoezi hilo limeshindwa
kuendelea baada ya watu wanaodaiwa kuwa ndiyo wenye mashamba ambao kwa awali
walikuwa hata 20 hawafiki lakini siku ya leo wameongezeka na kufika zaidi ya 60
huku wakitaka nao waorozeshwe kwenye uhakiki wa viwanja hivyo.
Hali hiyo ikatibua mambo kwani japo la wajumbe wa nyumba kumi
wakiongozwa na mwenyekiti Peter waligoma matakwa ya upande huo wa pili kutaka
kupachikwa watu hao ambao hwatambuliki, lakini hata hivyo katika hali ya
kushangaza maafisa Ardhi hao wakiongzwa na Seif walikuwa wanalazimisha watu hao
wasiofahamika wawekwe tu ili zoezi liendelee.
Msimamo mkali wa mwenyekiti wa Serikali za mtaa na kamati
yake kuwakataa watu waliokuwa wamepandikizwa ndiyo umepelekea watu wa ardhi
kuchukia pamoja na wale wa upande wa mafisadi kuamua kuondoka eneo la viwanja
hivyo na kupelekea zoei la uhakiki kusimama kuanzia leo hadi wananchi hao
watakapotangaziwa tena.
JUHUDI ZA MAKONDA ZINAVYOKWAMISHWA NA KIGOGO MWENYE NGUVU
KULIKO YEYE.
Katika jitihada za mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kuhakikisha
mgogoro huo unamalizika kwa amani na isitokee tena watu wakauna kama katika
eneo hilo zinadaiwa kukwamishwa na mtandao mkubwa ulimzunguka Makonda ambao
ukiongozwa na Mkuu wake wa kazi mwenye nguvu kuliko yeye huku akiwapa nguvu
watu wa Mipango miji, maafisa Ardhi, pamoja na msaidizi wake ambae wakazi hao
wanasema hawataki kumuona kwa vile wanajua kila kinachoendelea kuhusu mgogoro
huo.
Changamoto nyingine anayokutana nayo DC huyo ni kwamba
mgogoro huo ameukuta unaendelea na mbaya zaidi baadhi ya watumishi wa Manisptaa
wenye kitndo cha Ardh na Mipango miji wamekuwa sehemu ya mgogo huo na inadaiwa
walishavuta pesa ndefu toka kwa mafisadi hao ili kuhakikisha wanapata eneo hilo
kwa nguvu yoyote.
Bahari zaidi toka kwa vyanzo hivyo viliendelea kuueleza
mtandao wa maskanibongotz kuwa maafisa
hao wanatajwa kwenye kashfa hiyo wametokea kumchukia DC MAKONDA kwa kitendo
chake cha kuonesha kuwatetea wakazi hao
hali inayopelekea kushindwa kumpa ushirikiana na kama wanampa basi kwa
shingo upande, na mbaya zaidi yupo kigogo mmoja ambae ana sauti kuliko Makonda
kutokana na kuwa karibu na mafisaidi hao
wanaodaiwa kumwaga pesa kama mchanga.
Hali hiyo sasa inapelekea zoezi hilo kuwa na ugumu kutokana
na maafisa mipango na Ardhi kulindwa na boss wake Makonda, hata hivyo wakazi
hao wa NAKALEKWA na NAKASANGWE walionesha wasi wasi wao na hali ya usalama wa
Mkuu wao wa Wilaya juu ya jambo hili kwani tayari kwa sasa Dc huyo yupo kwenye
vita kubwa kupambana na boss wake, watu waliochini yake na mafisadi.
Kufuatia hali hiyo wananchi mbalimbali wanaofatilia mgogoro huu wa
kipindi kirefu wamemuomba Rais Dokta John Pombe Magufuli kumuongezea nguvu DC
Makonda kwenye sula hili kwa vile hali ya usalama juu ya jambo hili kwa sasa
kuwa mbaya kwani mkuu huyo anapambana hadi na bosi wake mwenye nguvu kuliko yeye i ambae anadaiwa
kuwapa nguvu watu wa ardhi na mipango miji kuhakikisha wanakwamisha hili
jambo.
Habari zaidi zilisema kuwa hata siku Makonda alipowaweka
ndani watu hao wa Ardhi na kutowaachia hadi kwa amri yake dakika
chache baadae ilidaiwa bosi wake Makonda alipiga simu na kuamuru waachiwe
haraka maafisa ardhi hao.
Kigogo huyo pia amewahi kusababisha mgogoro wa watu wa
gereji pale Tegeta kwa kutaka kuwahamisha watu hao hali iliyozusha balaa kubwa
kwani kigogo huyo ana rafiki yake muhindi ambae ndiye aliyekuwa anapataka pale
kwa watu wa magereji si kama alivyokuwa ametangaza kuwa wamevamia eneo la
hifadhi.
Mtandao huu unaungana na watanzania wapenda amani, wapenda
haki kuiomba Serikali
Kuu kwa maana ya Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim
Majaliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimwa Dk John Pombe
Magufuli kusikia kilio cha wapiga kura wake, lakini pia kuruhusu vyombo husika TAKUKURU kuchunguza tuhuma hizi
zinazowakabiri maafisa Ardhi, Mipango Miji na msaidizi wa DC Kinondoni ili kama
zina ukweli ndani yake basi wachukuliwe hatua haraka ili kuepusha uvunjifu wa
amani.
Na mahara pa kuanzia ni kule shamba kwani mambo yote yapo hadharani kwa mujibu wa wanakamati wanapambana na upande wa watu wenye mashamba na waliontwa wavamizi na huko watapata picha halisi ya tukio hilo la tuhuma nzito ambazo wananchi wanasema watumishi hao ni kama wanamshika masharubu Rais Magufuli ambae hapendi rushwa na ameapa kupamba nayo kwa mtu yeyote.
Na mahara pa kuanzia ni kule shamba kwani mambo yote yapo hadharani kwa mujibu wa wanakamati wanapambana na upande wa watu wenye mashamba na waliontwa wavamizi na huko watapata picha halisi ya tukio hilo la tuhuma nzito ambazo wananchi wanasema watumishi hao ni kama wanamshika masharubu Rais Magufuli ambae hapendi rushwa na ameapa kupamba nayo kwa mtu yeyote.
Mwandishi wa maskanibongotz siku ya aleo alifika ofisi ya Mkuu wa Wilaya
Kinondoni kwa ajiri ya kuzungumza na Mkuu huyo wa Wilaya kuhusu changamoto hizo
na tuhuma zinazowakabir maafisa wake wa ardhi na mipango miji hadi wananchi
kuwakataa lakini mkuu huyo hakuwepo ofisini na tulielezwa yupo nje ya ofisi kwa
kwa majuku ya kiofis.
Source:maskanibongotz
0 comments:
Post a Comment