Friday, November 27, 2015

Maiti zaidi ya 35 zapatikana, miezi minne baada ya mashambulizi ya Boko Haram Nigeria!


Mara ya mwisho kusikia headlines za matukio ya Boko Haram, Nigeria ilikuwa miezi kadhaa iliyopita na eneo la mwisho kusikia Boko Haram wapo lilikuwa Jimbo la Bama State… lakini leo kuna headlines mpya kuhusiana na jimbo hilo.
Zaidi ya maiti 35 iliyofukiwa kwenye maeneo ya jimbo la Bama imegundulika na Serikali za Mtaa miezi minne baada ya Jeshi la Nigeria kufanikiwa kuondoa vikosi vya Boko Haram katika eneo hilo.
Boma2
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa eneo husika, Ali Guija amewaambia waandishi wa habari jana November 26 2015 kuwa maiti hizo zilipatikana kwenye nyumba nyingi zilizoharibiwa na Boko Haram kwenye mashambulizi waliokuwa wakifanya kwenye mitaa ya jimbo hilo.
>>> “Tumefanikiwa kupata maiti zaidi ya 35 kwenye Jimbo la Bama kwenye zoezi la usafi tulilokuwa tunafanya maeneo hayo baada ya kupewa kibali na Serikali kusafisha mitaa ya Jimbo hilo ili kutoa nafasi ya kufanya ukarabati wa nyumba zilizoharibiwa ili watu waweze kurejea makazi yao ya zamani
Boma
source: www.lindaikejisblog.com.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king