Msanii Manaika Sanga akiwa na mashabiki wake walimuomba wapige picha nao huko Zanzibar ambako yupo kuangalia mwenendo wa mauzo ya filamu yake Iitwayo Wake Up pamoja na kuwasaka wezi wa kazi za wasanii kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoani humo
Mmoja wa mashabiki wa Manaiki akiwa kwenye picha ya pozi |
Msanii Manaika Sanga akiwa na mashabiki wake ambao ni wapemba wakifurahia baada ya kumuona msanii huyo live, Manaiki Sanga amejichukulia umaarufu mkubwa na heshima baada ya kutoka kwa filamu ya Wake Up
Msanii Manaika Sanga wiki iliyopita alizikonga nyoyo za mashabiki wake huko Zanzibar baada ya kufanya ziara ya kushtukiza huku umati mkubwa wa watu ukimsonga japo kumshika mkono pamoja na kupiga nae picha za ukumbusho.
Manaiki Sanga ambae toka kwenye mtandao wake wa kijamii anasema kuwa bado anaendelea na msako kwa wezi wa kazi za wasanii ambapo amekuwa akifanya kimya kimya ili kubaini kama kuna watu au mtu atakuwa anahujumu mauzo ya kazi yake mpya ya Wake Up filamu ambayo hadi sasa imevunja rekodi baada ya kuuza nakala nyingi kuliko filamu yoyote.
Aidha msanii huyo aliendelea kutoa angalizo kwa wezi wa kazi za wasanii na kusema msako mkali bado unaendelea kushirikiana na maofisa wa Jeshi la Polisi ambao amekuwa akizunguka nao kila mahara na kama watafanikiwa kumkamata mtu basi huyo jela ina mwita
0 comments:
Post a Comment