RIP Mchungaji Christopher Mtikila…
Asubuhi ya Octoba 04 2015 taarifa ya Majonzi ilitufikia ambapo taarifa
yenyewe ilikuwa inahusu msiba wa aliyekuwa Mwanasiasa mkongwe na
Mwenyekiti wa chama cha kisiasa cha DP, Christopher Mtikila ambaye alifariki kwa ajali ya gari eneo la Msolwa, Chalinze Mkoa wa Pwani.
.
Mwili wa Marehemu umeagwa leo October 07
2015 kuelekea mkoani Njombe na watu mbalimbali wamejitokeza kuaga mwili
wa Marehemu katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam wakiwemo Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal pamoja na viongozi wengine wa Serikali na wanasiasa pia.
.
Mke wa marehemu Mchungaji Christopher Mtikila, Mama Georgia Mtikila.
.
.
.
.
Watu wakiwa wamepanga mstari kwa ajili ya kuingia kuaga Mwili wa Marehemu Mchungaji Mtikila katika Ukumbi wa Karimjee, Posta Dar es Salaam.
.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wwa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal akiingia Karimjee kwa ajili ya kuaga Mwili wa Marehemu Mtikila.
.
.
.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ni miongoni mwa Viongozi waliofika kuaga mwili wa marehemu Christopher Mtikila.
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiondoka katika viwanja vya Karimjee baada ya kuaga mwili wa marehemu Christopher Mtikila.
.
.
.
.
.
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHAUMMA, Hashim Rungwe.
0 comments:
Post a Comment