Wasanii wengi wa Marekani sio washabiki wakubwa wa website ya TMZ na mmoja ya wasanii hayo ni R&B Superstaa Chris Brown.
Chris Brown amekuwa akisikika sana akiwashambulia TMZ kwa taarifa wanazo ziandika juu yake ambazo kwa asilimia kubwa amekuwa akizipinga… inaonekana time hii Chris Brown kakerekwa tena na taarifa za TMZ na kuamua kumshambulia muanzilishi wa site hiyo Harvey Levin kupitia page yake ya Instagram!
TMZ wanadai kuwa Chris aliivunja mkataba kati yao baada ya msanii huyo kutokutokea kwenye tamasha la Black Gay Pride Event jijini Atlanta siku ya tarehe 7 September mwaka huu…
Chris Brown
amepinga taarifa hizi na kudai kuwa wala hakuambiwa au kufanyiwa
booking yoyote ya tamasha hilo… pia amemshambulia muanzilishi wa website
hiyo Harvey Levin na kusema “kwasababu yeye ni shoga basi angekuwa anahangaika kutafuta njia za kuwasaidia mashoga wengine” na sio kuandika uongo juu yake!
Kupitia Instagram yake Chris alipost picha na ujumbe mrefu kuwasema TMZ…
“Jamani TMZ ifike hatua muache kuandika mambo ya kijinga…sijawahi
kuwekwa booking! Mnapenda sana kusema kuwa siwapendi mashoga ili kupata
tu sababu ya kuniongelea… sijali kama wewe ni shoga Harvey… badala ya
kuandika vitu unavyoviandika unatakiwa uwe unatafuta namna ya kuwasaidia
watu kama wewe ambao wanaona aibu kusema wapo vile walivyo… emu jaribu
kurekebisha focus wa webite yako…” <<< @chrisbrownofficial.
0 comments:
Post a Comment