Afisa Mawasiliano na mwanasheria Mkuu wa Kampuni ya E-fm Radio Co.LTD Dennis Sepo akifafanua jambo kwenye moja ya mikutano ya waandishi wa Habari |
Mtangazaji anaetarajia kuzolewa na mafuriko soon Gea Habibu toka kituo cha Clouds Fm Dar es Salaam
Mkurugenzi wa kituo cha E-fm Radio Jean Cloud Ciza
Na Shabani Fugusa Ripota wa Maskanibongotz
Raio ambayo kwa sasa imekamata namba moja Jijini Dar na mikoa jirani ya E-fm 93.7 huku mashabiki wengi kwa sasa wakiibatiza jina la UKAWA namba 2 kutokana na watangazaji wengi kukimbilia huko baada ya kuridhishwa na unono.
Habari za uhakika toka kwa vyanzo vyetu makini vya habri vilisema kuwa baada ya wiki iliyopita kumchukua mtangazaji mwenye kipaji cha hali ya juu Dinna Marius ambae alikuwa sambamba na mtangazaji mwenzake na mwandishi Gea Habibu kwenye kipindi cha Hekaheka, lakini sasa Gea amedaiwa yuko njiani kujiunga na mtangazaji mwenzake.
Habari hizo ambazo hazina hata chembe ya shaka zilisema kuwa Gea tayari ameanza mazungumzo ya chini kwa chini na uongoziwa E-fm Radio na huenda siku yoyote akadondoka.
Maskanibongotz ilifanya jitihada za kuutafuta uongozi wa kituo cha Clouds Fm kupitia kwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba ili azungumzie madai hayo ya mafuriko lakini kwa bahati mbaya simu yake iliita tu bila kupokelewa.
Lakini kwa upande wa kituo cha E-fm Radio alipatikana Sebo lakini hakuwa tayari kuzungumzia madai hayo kwa kusema ni mapema.
Hata hivyo pia mtandao huu ulimtafuta mtangazi Gea ili athibitishe taarifa hizo lakini simu yake iliita bila kupokelewa hadi habari hii inawafikia mamilioni ya wasomaji wetu Duniani.
Credit; maskanibongotz
0 comments:
Post a Comment