bofya hapa kuona filamu ya Goingi Bongo ambayo imewadatisha mastaa wengi wa bongo movie kiasi cha kumuweka mtu kati staa wa filamu hiyo Ernest Napoleon
Na Mwandishi Maalum
Mjini
bwana kuna mambo mengi sana hasa ukijichanganya kwenye viunga flani
flani vya burudani utasikia yanasemwa mazito na usiyoyatagemea, ambapo
kwa sasa habari mpya ya mjini ni juu kijana Ernest Napoleon ambae
makazi yake nchini Marekani lakini ni mtanzania ambae kwa sasa yupo hapa
mjini kwa mapumnziko mafupi.
Ernest
Napoleon ni staa wa filamu ya Kimataifa ya Going Bongo imeelezwa kuwa
kwa sasa anadaiwa kuwa kwenye mahusiano mazito na staa wa Bongo Movie
Wema Isack Sepetu hayo yanasemwa na watoto wa mjini wanaofatilia maisha
ya mastaa kwa kila kukicha, Gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita
ilipita katika kiunga cha starehe cha Maisha Basement maeneo ya
Makumbusho na kuzinyaka nyepesi nyepesi hizo toka kwa wadau hao.
Vyanzo
hivyo vya habari vilieleza baada ya kumuona Ernest Napoleon akiingia na
ndinga ya kinyamwezi VOUGE yenye namba za usajili CBK 859 katika
viunga vya Club hiyo huku gari hiyo ikiwa na vioo tinted ya ukweli
ambayo hata ukisogea jirani huwezi kuona kilichopo ndani lakini watu
wataalam bwana walipenyeza macho na kuona bint mrembo ambae wengi
walisema alihisiwa ni Wema Sepetu.
Hata
hivyo paparazi wetu ambae baada ya kusikia minong'ono hiyo alikurupuka
toka ndani nusura ateleze kwenye ngazi ndefu zilizopo kwenye Club hiyo
iliyopo chini kabisa na kusogea karibu ili nae asipitwe na taarifa hizo
na na kushuhudia gari hiyo yenye thamani ikiwa ikiwa inanguruma zaidi
ya masaa manne bila watu kushuka.
Habari
zaidi juu ya tukio hilo zilieleza kuwa gari hiyo iliingia maeneo hayo
majira ya saa tatu usiku hadi saa saba usiku baadae Ernest Napoleon
alishuka na kuelekea mahara wanapouza chakula ndani ya Club hiyo na
baadae alirejea na kuingia tena ndani ya gari kisha iliondoka na
kuelekea maeneo ya Mikocheni kupitia zilizpo ofisi za Mlimani Tv.
Baada
ya tuki hilo mmoja wa watu wa karibu na Ernest Napoleon alimwambia
mwaandishi wetu kuwa msanii huyo yupo kwenye mahusiano ya karibu na Wema
Sepetu bila kufafanua ni uhusiano upi haswa waliokuwa wasanii hao wenye
jinsia mbili tofauti, hiyo imekuja baada ya Ernest Napoleon kung'ara na
filamu yake ya Going Bongo ambayo hadi sasa imeshaoneshwa zaidi ya nchi
saba Duniani zikiwemo nchi ya China, Ujerumani, Uturuki, Marekani,
Uingereza, Kenya na nchi nyinginezo ikiwemo Nigeria.
Aidha
habari nyingine toka kwa vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa mastaa
wengi wa kike hasa wa bongo movie wamekuwa wakipigana vikumbo kuwa
karibu na msanii huyo tangu siku filamu hiyo iipooneshwa kwa mara ya
kwanza nchini Tanzania huko Zanzibar na kufanikiwa kuchukua tuzo ya
filamu bora Afrika Mashariki na kati, mastaa hao waliotajwa kujiweka
karibu ni Lulu Michael,Joketi Kidoti, Irene Uwoya, Jackline Wolper na
Dvj Penniel ambae kwa muda mrefu alikuwa mafichoni toka abwage manyanga
kwenye kituo cha E-fm Radio 93.7 alichokuwa anatangaza.
Joketi
na Ernest Napoleon walianza kutia shaka toka siku ilipooneshwa filamu
hiyo kwenye ZIFF, Kidoti alishindwa kujizuia ambapo mara ya kumalizika
filamu hiyo alimfuata Ernest na kumkumbatia pamoja na kumbusu kiasi cha
kuwashtua watu huku akimpongeza msanii huyo kwa kazi nzuri ya kimataifa
lakini cha zaidi Kidoti alimwambia Ernest kuwa hakuamini kama filamu
hiyo imeigizwa na mtanzania kutokana na kuwa na hadhi ya juu sana na kwa
haraka mtu huwezi huwezi amini.
Gazeti
hili lilianza kumtafuta Ernest Napoleon kupitia simu yake ya kiganjani
ili kuthibitisha madai hayo yote juu ya mahusiano hayo ambapo
alipatikana na kuelezea ukweli wa mambo na swali la kwanza lilikuwa
kutaka kujua mahusiano yake na Wema yakoje jibu lake ni hili " Kaka
mbona mimi sielewi unamaanisha nini? kwani mimi namfahamu Wema kama wewe
unavyomfahamu si vinginevyo" Alijibu Ernest, Lakini gazeti hili pia
liliuliza kama mtu aliyekuwa nae usiku pale Club ndani ya gari alikuwa
nani majibu mengine.
Credit:Maskanibongotz
0 comments:
Post a Comment