Sunday, November 2, 2014

MASKINI YA MUNGU: ANGALIA PICHA ZA TUKIO LA JAJI WARIOMBA ALIVYONUSURIKA KUCHEZEA KICHAPO TOKA KWA WAFUASI WANAODHANIWA KUWA NI WA CCM. AOKOLEWA. MAELFU YA WANANCHI WAMTIA MOYO WAMWAMBIA WAKO NYUMA YAO HADI KIELEWEKE..!


Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba akisaidiwa kutolewa katika vurugu






Na Sakina Shabani- Chuo Kikuu Dar Salaam
Katika mazingira ya kutatanisha, siku ya Jumapili vurugu zimekatisha mdahalo uliokuwa ukiendelea kujadili mchakato wa katiba mpya ya Tanzania huku baadhi ya watu wakipigwa na kujeruhiwa.
Mdahalo huo uliokuwa ukitangazwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni ulivurugika kutokana na kundi la vijana wapatao 20 kuanza kumzomea aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha mada yake.
Vijana hao ambao haijajulikana walitokea wapi au walikuwa na ajenda gani waliinua mabango ya kupinga msimamo wa waliokuwa wakiendesha mdahalo na kusema rasimu ya katiba iliyopendekezwa inakidhi mahitaji yote na kusema hakuna haja ya mdahalo.
Jaji Warioba ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania alifanikiwa kutoka nje ya ukumbi ulipokuwa ukifanyika mdahalo huo mjini Dar Es Salaam, lakini wapo watu waliojeruhiwa kutokana na kurushwa viti na vitu vingine.
Kiongozi wa kitengo cha hamasa umoja wa vijana CCM (UVCCM), Paul Makonda, aliyekuwepo ukumbini alidaiwa kuhusika na vurugu. Lakini alipoulizwa na na Maskanibongotz na alikuwa na haya ya kujibu tuhuma hizo Bw Makonda amekanusha kuhusika nazo huku akisema kwamba alihudhuria mdahalo kwasababu ulikuwa wazi kwa kila mtu.
Wakati wa vikao vya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, Makonda aliwahi kutoa kauli za kumkebehi Jaji Warioba ambaye tume yake iliandaa rasimu ya iliyokuwa ikijadiliwa na bunge hilo.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, aliieleza vyombo vya habari  kuwa hana maelezo ya kutosha na kwamba atalizungumzia akipata taarifa rasmi ya kiofisi.
CREDIT:MASKANIBONGOTZ

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king