Tuesday, October 21, 2014

UGONJWA WA MOYO WACHUKUA UHAI WA MSANII HUYU, ALITESEKA ZAIDI YA MIEZI TISA HADI UMAUITI WAKE. NI PIGO BONGO COMEDY ALIKUWA MPATANISHI KATI YA BONGO MOVIE NA KOMED..!


 DADAANGU UMENIACHIA UKUMBUSHO WA PICHA HII NILIYOKUPIGA MWAKA 2010 WAKATI FANYAKAZI GAZETI LA SANI. MUNGU AKUREHEMU...!


Na Livingstone Mkoi
Ni mtoto wa msanii nguli wa filamu na maigizo nchini Mzee Thobisa Charles Magali anaitwa Sheri Magali ambae nae alikuwa msanii wa maigozo na Komedi ambae sasa ni ametuacha baada ya kufariki kufuatia kuugua kwa muda mrefu.
Shery Magari alianza kuugua miaka miwili iliyopita akisumbuliwa na ugonjwa wa Moyo ambapo familia yake ilihangaika sana kunusuru maisha yake lakini ilishindikana ambapo mamilioni yamepotea kwa ajili ya kunusuru maisha yake lakini Mungu amempenda zaidi.
Binafsi: Nilimfahamu Shery kupitia harakati zake za upatanishi wa ubaguzi uliokuwepo kipindi flani kati ya wasanii wa Bongo Movie na Bongo Comedy ambapo msanii huyo alifanya juhudi za pekee kuhakikisha wasanii wa Comedy wanapata heshima yao na kuacha kuchezeshwa seen za kufungua mageti wakati wasanii Bongo Movie wao wakiwa na seen za heshima.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king