Browse » Home
Monday, July 18, 2016
RC MAKONDA AFAFANUA ALICHOMANISHA KUHUSU MSAKO WA NYUMBA KWA NYUMBA KUIBAINI WAKAZI NA MAJUKUMU YAO, WANASIASA WANAOMPINGA WAWACHUKIZA WANANCHI..!
Na Livingstone Mkoi
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda ametolewa ufafanuzi kuhusu upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa kisiasa dhiti ya maagizo mbalimbali anayokuwa anayatoa kwa ajiri ya kuijenga Dar Es Salaam mpya.
Akiongea na mtandao wa maskanibongotz Mheshimiwa Makonda alisema "Sikusema wasio na kazi wakamatwe. Utawapeleka wapi? Una gereza gani? Nilisema Wenyeviti wa mitaa wahakikishe wanawafahanu watu wao vizuri na shughuli wanazofanya. Wakitilia shaka nyumba fulani wachukue polisi kukagua na sio kukamata wasio na kazi kama inavyopotoshwa.." Alisema Makonda
Aidha Mkuu huyo wa mkoa aliongeza kusema kila agizo alilolitoa litakwenda kutekelezwa na kuhusu na tayari vyombo vya usalama hasa Jeshi la Polisi limeanza kutekeleza agizo la Serikali.
Aidha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kinondoni Christopher Fuime aliueleza mtandao huu kuwa tayari wanashikiria vifaa vya shisha pale Oysterbay Polisi na msako mkali unaendelea kukamata machangudoa kwenye madanguro na wa barabarani ili kutimiza agizo la RC Makonda.
Hata hivyo wakazi wengi wa Jiji la Dar wamesikitishwa na kauri ya Meya wa Jiji la Dar aliyoitoa hivi karibuni ya kupinga agizo la Makonda ambalo kiukweli liko wazi na linaonekana kuwa na faida kwa jamii nzima ya Dar kwani mfano agizo la kuorozeshwa kwa wakazi wote kwenye nyumba wanazoishi na majukumu yao hali hiyo italeta faida kubwa kwani uharifu umekuwa mwingi kutokana na watu kuishi kiholela.
Wananchi hao wameomba wanasiasa kuacha kuacha kuingilia majukumu yenye faida kwa watu wengi kuliko wao wanasiasa wachache.
Paul Makonda (RC Dar).!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment