Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob "UKAWA"
Mheshimiwa Halima Mdee Mbunge wa Kawe- CHADEMA
Mkuu mpya wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi Salum
Isaya Mwita wa Chadema, Meya wa Jiji la Dar es Salaam "UKAWA"
Na Mwandishi wa Maskanibongotz
Mashabiki na wafuasi wa vyama vilivyoungana UKAWA wamekuja juu na kuwataka viongozi wao wanashikiria nyazifa mbalimbali za kuwaongoza wananchi waachane na maneno badala yake wapige kazi ionekane ili wananchi waendeee kuwa na imani nao.
Wakiongea na mwandishi wetu juzi maeneo ya Kinondoni jirani na yalipo makao makuu ya Chadema walisema kuwa " Ndugu mwandishi sisi ni wafuasi wa Ukawa lakini kwa sasa tunachowataka viongozi wetu waingia mtaani kutatua matatizo ya wananchi na kero zao kwa vile wanamamlaka ya kufanya hivyo kutokana na nafasi walizonazo" Alisema
Timoth Nyang'andu ambaye anatokea mkoani Singida.
Wafuasi hao waliongeza kusema kuwa kwa sasa viongozi hao waachane na habari za malumbano na Mkuu wa Mkoa wa Dar kwa kupinga kauri anazozitoa kwa maana kufanya hivyo ni sawa kama wamekosa mawazo endelevu ya kuwasaidia wananchi.
Mashabiki hao wameomba Mwenyekiti wa Chama hicho Kitaifa Mheshimiwa Freeman Mbowe atumie mamlaka aliyonayo kuwasihi viongozi waliopo chini yake nchi nzima kuachana na malumbano wapige kazi 2020 sio mbali kwani CCM wanajipanga kurudisha nafasi hizo hivyo njia watakazopitia CCM ni kuangalia mapungufu yaliyofanywa na Mamea hao nk.
Wakipiga mfano mgogoro wa Nyaksangwe kata ya wazo ambao kimsingi ni kama umemalizika kutokana na pande zote kati ya wenye mashamba na wakazi hao kukubaliana kumaliza hivyo ni nafasi pekee ya mamea Isaya Mwita wa Chadema, Meya wa Jiji la Dar es Salaam "UKAWA"
Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob "UKAWA" na Halima Mdee wanaweza kutumia nafasi hii vizri ya kushika nyazifa hizo kumaliza mgogoro huo uliouwa watu wengi sana miaka 7 iliyopita.
Halima Mdee Mbunge wa Kawe mgogoro huu unamuhusu sana kutokana na kuwa eneo lake na anaufahamu vizri mgogoro huu na anajuwa kabisa kama wapiga kura wake waliwahi kupoteza maisha wakigania haki yao hivyo ahusishwe pamoja kumaliza tatizo hilo ambalo Mheshimiwa Makonda walishaweka njia nzuri ya kumaliza mgogoro huo.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni Boniface Jacoblicha ya hivi karibuni kufanya ziara ya kushtukiza kwenye eneo hilo lenye mgogoro na kupokelewa na maelfu ya watu na kujione auharibifu mkubwa uliofanywa na mafisadi ardhi hao waliotumia pesa zao kuwaangamiza wananchi hao kwa kutumia Jeshi la Polisi na mabaunsa na aliahidi kama miezi miwili isingepita ofisi yake ingeanza kugawa hatimiliki ya viwanja hivyo kwa kila mkazi mwenye eneo hilo ili watu wawe na uhakika na viwanja vyao lakini hadi leo kimya.
Source: Maskanibongotz
0 comments:
Post a Comment