Monday, May 2, 2016

RC MAKONDA KIBOKO, MAFISADI WA ARDHI KATA YA WAZO WAINGIWA HOFU YA KUKAMATWA, NI WALE WANAOKABIRIWA NA KESI YA KUUA WATU, KUHARIBU MALI ZA WANANCHI WANYONGE, KUIDANGANYA MAHAKAMA...!

 DC Makonda akipokewa na mabango ya kuwakataa maafisa Ardhi Manspaa ya Kinondoni wanaidaiwa kuwa karibu na mafisadi hao
 Hapa picha hii Makondo akiwa amekaa chini siku ya kwanza alipotembelea Nyakasngwe akiwa DC

Na Mwandishi wa Maskanibongo- Wazo
Hakika serikali ya awamu ya tano imerejesha matumaini mengi ya watanzania hasa wanyonge waliokuwa wanaonewa na watu wenye fedha zao makusudi huku wakikosa mahara pa kukimbilia, huku wananchi wengine  kupoteza maisha kwenye harakati za kutetea haki zao, moja ya eneo ambalo lilikuwa na vita kubwa ni Nyakasangwe kata ya Wazo ambalo mafisadi walilitumia kuwafanyia watu umafia wa kutisha.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda wakati akiwa bado mkuu wa Wilaya ya Kinondoni aliingilia kati sakata la mgogoro huo wa ardhi kati ya watu wanaojiita wenye mashamba na wananchi wakati wa eneo hilo kupitia maamuzi yake alifanikiwa kurudisha amani iliyokuwa imepotea muda mrefu kwenye eneo hilo.
Makonda atakumbukwa na wananchi wanyonge wa eneo hilo kwa kuwatetea na kuwatia moyo wakati akiwa mkuu wa Wilaya hali hiyo iliwafanya watu wanaodai ni wamiliki wa mashamba hayo kumuangalia kwa jicho mbaya Makonda kwani awali mafisadi hao walizoea kuwatumia viongozi wa Serikali hasa wa awamu iliyopita kwa kutoa rushwa ili wawakatandamize wananchi.
Makonda katika sakata hilo alionesha msimamo wake hali iliyopelekea mafisadi hao kumuogopa sana huku wengi wao walianza kuyaacha wazi maeneo hayo ili wananchi hao waendelee kuishi kwa amani na utulivu.
Hata hivyo kwa sasa hali imekuwa mbaya licha ya kwamba kesi ya mgogoro huo wa ardhi ipo mahakamani, upande wa pili mafisadi hao wameingiwa na hofu ya kukamatwa kwa mambo matatu, Jambo la kwanza wana kesi ya kuidanganya mahakama kwa kusema wanamiliki maeneo yenye ukubwa flani lakini kumbe ni uongo. jambo la pili katika mgogoro huo kuna wananchi wanyonge walipoteza maisha na jambo la tatu mali zao ziliharibiwa na polisi huku kazi hiyo ikifanywa na mafisadi hao.
Hivyo kutokana na hali hiyo imelezwa kuwa mafidi hao kwa sasa wanaomba kuyamaliza nje ya mahakama ili kukwepa kitanzi hicho, ambapo imelezwa tayari Makonda ana ripoti yote kwa sasa mezani na amebakisha kufanya maamuzi magumu juu ya mafisadi hao kwani hawakuwa na kibali toka mahakamani kuwabomolewa wananachi hao na kuharibu mali lakini na kusababisha maafa kwa wananchi.
Makonda ambae kwenye mgogoro huo wakati akiwa mkuu wa wilaya alishindwa kufanya maamuzi kutokana na vikwazo flani vilivyokuwepo toka kwenye ofisi ya mkuu wa Mkoa aliyepita ambapo ilidaiwa kuwa ilikuwa anahusika na mgogoro huo hivyo hali ilimfanya Makonda kushindwa kufanya maamuzi ya mwisho lakini kwa sasa kapewa rungu na mheshimiwa Rais  la kufanya maamuzi watanzania wengi wanatarajia kuona mafisadi hao wakichukuliwa hatua kali.
Source: maskanibongotz

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king