HAPA MKUU WA KITENGO CHA HABARI ZA UCHUNGUZI TOKA E-FM RADIO 93.7 KULIA BW LIVINGSTONE MKOI AKIONESHWA MLIMA AMBAO NG'OMBE HAO WALIOGEUKA FISI WALIPOKIMBILIA BAADA YA KUGEUKA KUWA FISI MKOANI TABORA NA ANAETOA MAELEKEZO HAYO NI KIJANA ALIYEKUWA AKIWACHUNGA NG'OMBE HAO WA KICHAWI.
HAWA NI BAADHI YA NG'OMBE HALALI WALIOBAKI BAADA YA WENGINE KUGEUKA KUWA FISI.
MAHARA HAPA NI SEHEMU YA ZIZI LA NG'OMBE WALIOKIMBILIA MSITUNI BAADA YA KUGEUKA KUWA FISI KWENYE KIJIJI CHA UKANGA WILAYA SIKONGE MKOANI TABORA
MCHUNGAJI WA NG'OMBE HAO ALIYEJITAMBULISHA KWA JINA LA MUSA MAJIHA AKIHOJIWA NA MWANDISHI WETU BW LIVINGSTONE MKOI HAYUPO PICHANI
DOKTA KAMDEGE MTAALAMU WA MITI SHAMBA AKIWA NJE YA OFISI YAKE MKOANI TABORA TAYARI KUELEKEA KWENYE KIJIJI KISANGA NJE KIDOGO YA WILAYA YA SIKONGE KWA AJIRI YA MPAMBANO NA KUWATOKOMEZA FISI HAO.
HII NDIYO OFISI YA DOKTA KAMDEGE KAMA INAVYOONEKANA.
Na Waandishi wa maskanibongotz- Tabora
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya filauni hivi ndivyo tunavyoweza kusema kufuatia mzee mmoja Mkoani Tabora amekuwa akiwanywesha watu maziwa ya Fisi zaidi ya miaka 25 sasa, huku watu wengi wakidhani ni Ng'ombe huku maziwa hayo yakiwa matamu kupita kiasi.
Tukio hilo la kushtua lililoripotiwa na kituo cha E-fm Radio hivi karibuni, ambapo katika habari hiyo wakazi wa Kijiji cha Ukanga kilichopo Wilaya ya Sikonge wakimlalamikia mzee huyo wa kisukuma kwa tukio alilowafanyia.
Habari zaidi zilieleza kuwa mtaalamu wa miti shamba Dokta Kamdege ndiye aliyegundua kuwa maziwa hayo si halali baada ya wananchi eneo hilo kumuita mtaalamu huyo kwa ajiri ya kuwasaidia mambo mengine lakini akiwa huko aligundua tatizo la maziwa hayo ya fisi.
Mzee huyo alikuwa na ng'ombe zaidi ya mia na hamsini huku ng'ombe halali wakiwa 50 tu na mia wakiwa ni fisi pamoja na watoto wao ambao kwa macho ya kwaida walikuwa wanaonekana ni ndama wa ng'ombe.
Hata hivyo baada ya mganga huyo kugundua hali hiyo wananchi waliitisha mkutano mkubwa na kumuomba mganga huyo awasaidie kuhusu tatizo hilo, ndipo alipokwenda kwenye zizi la mganga huyo lakini walikutana na mtihani mkubwa kwani mzee huyo alikuwa ametega umeme kwenye zizi hilo na ukamnasa mmoja wa wasaidizi wa Dokta Kamdege hadi kupoteza fahamu kwa muda kabla hajapatiwa huduma ya kwanza.
Kwa mujibu wa Dokta Kamdege alisema umeme huo ulikuwa wa kichawi kwani katika eneo hilo la polisi bado hakuna maendeleo ya umeme, hivyo ndipo walipomwaga dawa zake kisha ng'ombe hao walianza kugeuka fisi kisha kukimbilia polini na kubaki wale ng'ombe hamsanini halali.
Kutokana na tukio hilo kuna uwezekana Dokata Kamdege akahojiwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo ili kujua kama maziwa waliyokunywa wananchi hao yana madhara ama laa, kwani Serikali haiamni uchawi lakini yeye ndiye mtu aliyegundua hayo.
Akiongeo na matndao huu kwa simu namba 0788-844490 Kamdege alisama " Ndugu mwandishi haya ni mambo ya kishirikina hata mimi imenihudhunisha sana kuona wananchi wakinyweshwa maziwa ya fisi hali ambayo sisi tuliojaliwa na Mungu kuwa na vitu vyema kichwani ni lazima tuwasaidie na haieleweki kama watakuja kudhurika ama laa" Alisema Kamdege
Na pia alitoa uwito kwa watanzania mahali popote kama kuna mambo ya ajabu wanafanyiwa au wanahisi kama maisha yao hayaendi vizuri, mipango wanayoipanga hatimii basi wawahi kumjurisha ili awasaidie hayo yote yanafanywa kutumia miti shamba tu wala sio uchawi au ndumba, pia hata kukwamba kwa biashara. maradhi yalishindikana, kushindwa kupata kazi licha ya kwamba watu wengi wamesoma na kuwa na ujuzi lakini wabaya wameziba ridhiki basi hayo yote yanafunguliwa kwa dawa maalum za miti shamba.
Hata hivyo wananchi hao kwa nyakati tofauti walisema kuwa hadi sasa wana hofu kutokana na kunywa maziwa hayo kwa kipindi kirefu hivyo wasi wasi wao huenda yakawaletea madhara siku za usoni
Credit: Maskanibongotz
0 comments:
Post a Comment