Wednesday, February 24, 2016

MAFISADI WA ARDHI KATA YA WAZO KWENDA JELA, DC MAKONDA AWAWEKEA MTEGO WA AINA YAKE, WANANCHI ILALA, TEMEKE NA KINONDONI WABARIKI KUWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM..!


DC MAKONDA AKIWA AMEKAA CHINI NA WAKINA MAMA WA NYAKASANGWE KATA YA WAZI SIKU YA KWANZA KUWATEMBELEA WAKAZI HAO
Na Mwandishi Wetu
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati zoezi ambalo ni agizo toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda la kutaka kutafuta suruhu ya mgogoro wa ardhi kati ya watu wanaojiita wenye mashamba na wakazi mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa ulipo kata ya Wazo hatimae kuna dalili zote za watu wenye mashamba kukukutwa na hati ya kuidanganya mahakama, kuua bila kukusudia pamoja na kuharibu mali za samani ya mabilioni ya pesa.
Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa katika zoezi hilo kumeibua mambo mengi likiwemo suala la watu hao wenye mashamba kuongea uongo Mahakamani kwa kutaja ukumbwa wa maeneo yao tofauti na alichokikuta mkuu huyio wa wilaya kwani wengi wao  awali waliteja kuwa na maeneo makubwa lakini baada ya zoezi hili la uhakiki imegundulika kuwa wengi wao ni waongo.
Hata hivyo hali hiyo imemfanya mkuu wa Wilaya hiyo kwa sasa kushirikiana na vyombo vingine vinavyohusika kujipanga kwa ajiri ya kuchukua hatu zinazostahiri, ili iwe fundisho kwa  mafisadi wengine wa ardhi wenye tabia mbaya kama hizi za kuwaonea wananchi kwa kutumia pesa zao.
Aidha katika hatua hiyo wananchi wengi Jijini Dar wamemuomba Rais John Pombe Magufuli kumpa nguvu DC huyo kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwatetea wananchi wanyonge hasa wanaoonewa.
Wakati huo wakazi wa Jiji kwenye wilaya zote za Temeke,  ILALA na Kinonodoni wametoa Baraka zao kwa Dc huyo kama Mheshimiwa Rais kumpa Ukuu wa Mkoa wa Dar kwa vile kazi zake zinaonekana kwani pia Wilaya zote tatu zinamuhitaji na wanaimani nae.

 Mzozo wa Nyakasangwe ulipelekea wananchi zaidi ya 7 kufariki baada ya mafisadi hao kupeleka askari Polisi kuwavunjia nyumba zao.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king