Friday, February 5, 2016

AFANDE MACHEMBA AWARUKISHA KICHURA CHURA BONGO MOVIE, RAY NA JB, MASHABIKI WAWATAKA MASTAA HAO KUSTAAFU SANAA ILI KULINDA HESHIMA YAO...!


 AFANDE MACHEMBA
WASANII WENYE MAJINA NCHINI TANZANIA BONGO MOVIES TEAM




Na Mwandishi wa Maskanibongotz

Kipaji cha Msanii kinda kwenye tasnia ya Filamu Tanzania Joseph Machemba sasa kimeonekana kuwaamsha uzingizini mastaa wa kiume Vicent Kigosi"Ray" Na Jakobu Steven "JB" na wengine huku mashabiki wengi wakiwashauri Ray na Jb kuachana na sanaa kwa sasa.
Mashabiki hao wakiongea na maskanibongotz walisema kwa kipaji anachokionesha msanii Afande Machemba  hakika ni dhahiri kabisa anaweza kuifikisha sanaa ya Tanzania Kimataifa na sio kama Ray na Jb ambao kwa sasa wanasafiria nyota za zamani kwa kushindwa kufanya juhudi zozote za kuwa wa kimataifa. Mashabiki hao waliendelea kusema wamefurahishwa na upinzani mkali aliouonesha  Afande Machemba kwenye sanaa kwani kulizika kwa msataa walipo kungeweza kuleta athari kwenye sanaa hii kwani Ray na Jb uwezo wao ulishakufa tangu alipotangulia mbele za haki Marehemu Steven Kanumba hadi leo sanaa ya Filamu imerudi nyuma kwani hakuna hata staa mmoja ambae anaonekana ana kiu kama aliyokuwa nayo marehemu Kanumba ya kuifika sanaa ya Tanzania kimataifa.
Filamu zilizomtambulisha Afande Machemba ni Filamu alizoonekana Afande Machemba ni pamoja na, Karoge  Tena, Night Dress, Akiri Nyingi, Bifu la Kitongoji na ndani yake ameonesha kipaji cha hali ya juu kiasi cha kuwafanya mashabiki wanajiuliza kwa nini alikuwa amechelewa kuanza kuigiza.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king