Licha ya kuwa Jumapili ya November 8
kuna michezo kadhaa inapigwa barani Ulaya ila mchezo wa fainali ya pili
ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika ndio mchezo uliyokuwa umevuta hisia za
watu wengi barani Afrika hususani Tanzania ambao walikuwa wanasubiri kuwaona nyota wao Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wakiweka rekodi katika fainali hizo.
TP Mazembe ilicheza
mchezo huo wa pili ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa goli 2-1 katika
mchezo wa kwanza, huku ikiwa na rekodi ya kutwaa taji hilo kwa mara ya
mwisho mwaka 2010 na mastaa waliotwaa taji hilo katika mwaka huo
wamebakia watano pekee kikosini Given Sunguluma, Robert Mutebe Kidiaba, Aime Bakula, Joel Kimwaki na Jean Kasusula.
Mtanzania Mbwana Samatta
ambaye kabla ya mchezo huo kuchezwa alikuwa akihitaji goli moja pekee
ili aweze kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo kwani
alikuwa sawa na mshambuliaji wa klabu ya Al Merreikh Bakri Abdel Kader Babeker wote wakiwa na jumla ya goli 6 ila Samatta amefanikiwa kufunga goli la saba.
Mchezo umemalizika kwa TP Mazembe kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 2-0, kwa mara nyingine tena Mbwana Samatta amefanikiwa kufunga goli kupitia mkwaju wa penati baada ya Roger Assale kufanyiwa faulo dakika ya 74, USM Alger wakiwa katika jitihada za kusaka goli Mbwana Samatta alipata mpira kutokea katikati ya uwanja na kukimbia nao hadi golini na Roger Assale akapachika goli la pili na kuifanya TP Mazembe ichukue Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mwaka 2015 toka itwae Kombe hilo mara ya mwisho 2010 dhidi ya Esperence.
0 comments:
Post a Comment