Bondia mwenye rekodi ya kutopigwa Floyd Mayweather bado anaendelea kufanya matanuzi ya mkwanja wake aliyovuna katika mchezo wa ngumi. Floyd Mayweather ambaye mwezi September alimpiga kwa point bondia Andre Berto pambano lililofanyika katika ukumbi wa MGM Grand Garden Arena Las Vegas Marekani.
Mayweather Jr alipigwa picha akiwa katika bwawa la kuogelea Miami
sambamba na uwepo wa rafiki zake, huku akionekana kujiachia zaidi
dalili ambazo zinaashiria kuwa hana pambano hivi karibuni kwani muda
mwingi ameonekana akiwa anaenjoy na rafiki zake.
Bingwa huyo wa uzito wa kati hadi sasa
ana rekodi ya kupigana mapambano 49 na kutopoteza pambano hata moja kati
ya hayo. Hata hivyo kuna stori zinazozungumzwa kuhusu promota maarufu
wa mchezo wa ngumi Bob Arum kutaka kuandaa pambano la marudiano kati ya Mayweather Jr dhidi ya mpinzani wake Manny Pacquiao.




0 comments:
Post a Comment