Tuesday, September 15, 2015

KIMENUKA: WANANCHI KINONDONI WAMUOMBA RAIS JAKAYA KIWETE KUMUONDOA MAKONDA KWENYE NAFASI YA UKUU WA WILAYA KABLA HAJAONDOKA MADARAKANI, WASEMA MENGI KUHUSU DC HUYO, RPC WAMBURA NAE AHUSISHWA..!



RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIPEANA MKONO NA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MH PAUL MAKONDA

 MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MH PAUL MAKONDA AKIWAJIBIKA KWENYE MOJA YA MAJUKUMU YAKE HIVI KARIBUNI
MKUTANO WA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MH PAUL MAKONDA KATA YA NAKASANGWE TEGETA JIJINI DAR
  MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MH PAUL MAKONDA AKIZUNGUMZA NA WAKAZI WA NAKASANGWE KWENYE MKUTANO ALIOUANDAA YEYE MWENYEWE KUHUSU MIGOGORO YA ARDHI
  MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MH PAUL MAKONDA AKIWA AMEKAA CHINI PAMOJA NA NA WAKAZI HAO AMBAO KWA KIPINDI KIREFU WALIKUWA WANAISHI KWA HOFU NA MASHAKA KWA KUHOFIA KUPIGWA MABOMU NA POLISI KWA KILE KILICHOELEZWA KUWA WALIKUWA WAMEVAMIA ENEO HILO LA MWEKEZAJI JAMBO LILILOPIGWA NA WAKAZI HAO
 MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MH PAUL MAKONDA AKIWALINGANISHA WAKAZI HAO JINSI UWIANO ULIVYO KWA KATI YA MTU ALIYEKUWA NACHO NA ASIYEKUWA NACHO AKIPIGIA MFANO KUWA HUYO JAMAA MFUPI NDIYE MAKAZI WA ENEO HILO NA HUYO BAUNSA NDIYE FISADI ANAETAKA KUDHURUMU ENEO HILO.

 MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MH PAUL MAKONDA
Na Livingstone Mkoi
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua wakazi wa Kata ya Wazo na Nakasangwe wamemuomba Rais Jakaya Mrisho Kikwete kumuongezea cheo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa kile kilichoelezwa amewasaidia kuwarejeshea amani waliyoitafuta kwa zaidi ya miaka mitano.
Wakaiongea mwandishi wa E-fm Radio bwana Livingstone Mkoi kwenye mkutano wa hivi karibuni ulioandaliwana Mkuu huyo wa Wilaya ambae ni kipenzi cha watu walisema" Ndugu Mwandishi kwa sasa tunajiona ni watanzania halisi kwani hali ilikuwa mbaya kuhusu huu mgogoro wa ardhi ambao uliwasababishia umasikini mkubwa baada ya kubomolewa makazi yao na mali nyingi kuharibiwa" Alisema mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Dula

Mgogoro huo wa ardhi uliwaathiri wakazi wa eneo hilo ambao wengi wa wafuasi wa chama cha Mapinduzi CCM na kupelekea suala hilo kufika kwenye mamlaka za kisheria na walishashinda na walitakiwa kulipwa fidia lakini katika hali nyingine upande wa wa pili ambao wanadai ni wawekezaji walikata rufaa na kutaka kesi iendelee ambapo hadi sasa bado kesi hiyo inaendelea.
Mkuu wa Wilaya aliandamana na Mkurugenzi wa Manspaa ya Kinondoni, Afisa Ardhi wa Manspaa na maofisa wengine toka Wilaya akiwepo RPC Wambura na kwa kauri yake Mkuu wa Wilaya hiyo baada ya kupata maelezeo ya toka kwa wananchi ambao walimweleza wazi kuwa kufika hapo kwa mgogoro huo kulikuwa kumesababishwa na mkuu wa Wilaya aliyepita kabla yake ambae walimtuhumu kuwa alikuwa akishirikiana na mafisaidi kuwakangamiza wananchi pamoja na kutoa amri kwa jeshi la Polisi kuwabomolea nyumba zao na kuwalipua kwa mabomu ya machozi.

Hata hivyo katika mkutano huo Mkuu huyo kwa kauri yake alisema " Ndugu zangu kwanza niwashukuru kwa maelezo yenu kwani nilikuwa nimepata maelezo ya upande mmoja ambayo ni toka kwa wenzenu wanaodai haya ni maeneo yao lakini sasa nimepata picha halisi ya mgogoro huu ni dhahiri unaonekana una chembechembe za rushwa lakini mimi nawaahidi kuwasaidia na kuanza sasa naagiza Afisa Ardhi kushirikiana na Mwenyeketi wenu kwanza waje wapime eneo lote hili kisha tukishajua lina ukubwa gani basi tutapata picha halisi na namna ya kufanya bila kuingilia uhuru wa mahakama kwenye hiyo kesi nyingine inayoendelea" Alisema Makonda

Hivyo kutokana na Mkuu huyo wa Wilaya kuonesha moyo wa dhati wa kuwapigania wananchi hao wanyonge na kufuta kauri ambayo awali ilikuwa inatumiwa na viongozi wa Manspaa kuwa watu hao ni wakaimbizi kutokana na ukweli kwamba watu wote wanaoishi eneo hilo ni watanzania  halisi, wanchi hao walifarjika na kumuomba Raisi Jakaya Mrisho Kikwete kumuongezea cheo Mh Makonda na kumpa ukuu wa Mkoa kwa vile kwa kipindi kifupi alichooingia madarakani tayari amefanya mambo makubwa hasa kuhusu migogoro ya ardhi sehemu mbalimbali ya Wilaya hii hivyo wanaamini endapo akiwa mkuu wa Mkoa nadhani atahakikisha Mkoa mzima unakuwa na amani pamoja na vijana wengi kupata ajira.

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king