Add caption |
WALIOKUWA WASHIRIKI WA FILAMU YA MSANII MANAIKI SANGA IITWAYO WAKE UP WAKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA ! |
MSANII MANAIKI SANGA |
MSANII MANAIKI SANGA AKIWA NA STAA WA FILAMU YA KIMATAIFA YA GOING BONGO ERNEST NAPOLEON |
FEDHWAA ZA MNYAMWEZI
Na Mwandishi Wetu
Msanii Manaiki Sanga sasa huenda asikamatike tena kwenye sanaa baada ya kuzoa mamilioni ya Steps kwa ajir ya mauzo ya filamu yake ya Wake Up sasa hivi yupo mbioni kuikimbia Tanzania na kwenda kujichimbia Ulaya kwa ajiri kuandaa kazi nyingine mpya.
Habari zilizonaswa na mtandao huu zinasema kuwa msanii Manaiki Sanga kwa sasa ameungana na msanii Mtanzania anaeishi Sweden Ernest Napolion kwa ajir ya kuandaa kazi moja matata ya kutikisa dunia.
Hata hivyo alipotafutwa Manaiki kupitia simu yake ya kiganjani alisema hivi " Kaka hizo taarifa zimevuja haraka sana nani kakwambia hayo? Hii ilikuwa bado kwenye kapeti lakini huenda zikawa na uhakika ndani yake hivyo tuombeane heri tunaweza kuleta mabadiliko kwenye tasnia ya filamu Tanzania ama Afrika kutokana kwa sasa kuonekana inadidimia baada ya wasanii wanaojiita mastaa kuridhika na hali iliyopo huku fikra zao zikiwa zimefika mwisho" Alisema Manaiki Snga
0 comments:
Post a Comment