Friday, July 31, 2015

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI PAUL MAKONDA AFANYA MAMBO YA KUSHANGAZA HADI WANANCHI WAPIGWA BUTWAA. MASKANIBONGOTZ..!





 HAPA DC WA KINONDONI PAUL MAKONDA AKIWA AMEKAA CHINI YA ARDH AMBAPO MKUU HUYO WA WILAYA ALIACHA KUKALIA KITI CHAKE ALICHOKUWA AMEANDALIWA NA KWENDA KUKAA CHINI NA WAKINA MAMA WALIOKUWA WAMEKUJA KUMSIKILIZA KUHUSU MGOGORO WA ARDH ENEO LA NAKASANGWE LEO IJUMAA ALIPOTEMBELEA HUKO NA MAOFISA WAKE.


Katika hali ya kushtua na kushangaza mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda leo Ijumaa amewashangaza mamia ya wakazi wa kijiji cha Nakasangwe huko Tegeta Jijini Dar baada ya kuacha kukalia kiti badala yake ameenda kukaa chini kwenye vumbi pamoja na wakina mama waliokuwa wamekuja kumsikiliza wakati alipokuja kusikiliza mgogoro wa ardhi katika eneo hilo.
Mtandao wa Maskanibongotz ambao ulikuwa kijijini huko kushuhudia kikao hicho kilichokuwa baabu kubwa  kutokana na wanancha wa eneo hilo kuwashutumu maofisa ardhi kudaiwa kutumiwa na watu wenye pesa ili kuwakandamiza.
Hata hivyo katika kikao hicho Mh Makonda amesema atapigana kufa kupona ili wananchi hao wapimiwe ardhi yao ili waishi kwa amani.
Credit; Maskanibongotz

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king