Waziri mambo ya ndani ya Nchi Mathias Chikawe ambae ameombwa na wananchi wakazi wa Kitongoji cha Kinondoni Moscow kata ya Hananasif kutatua tatizo hilo la kuhamishwa mkuu wa kituo kidogo cha Polisi cha Hananasif aliyefahamika kwa jina Sajent Deogratus
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Suleiman Kova
Igp Ernest Mangu
Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete
Camillius
WamburaWananchi mbalimbali wanaishi Kinondoni Moscow Kata ya Hananasif wamemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Mathias Chikawe kumuondoa Mkuu wa kituo Kidogo cha Polisi cha Hananasif aliyefahamika kwa jina la
Sajent Deogratus kwa madai ya kuwanyanyasa kwa kauri mbaya na kuwafokea bila kuwapatia huduma.
Wakiongea na gazeti moja hivi karibuni wananchi walisema kuwa mkuu huyo wa kituo ambae ni mtu mzima amepelekea Wananchi kuanza kulichukia Jeshi hilo kupitia yeye kwa vile ameshindwa kuwa na ushirikiano nao hali inayoondoa amani katika kitongoji hicho.
Aidha wakazi hao walimaliza kusema wana imani na wakuu wa idara hiyo kwani licha ya Serikali za mtaa huo kuitia Mwenyekiti wao Selemani Rada kupeleka taarifa kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa ajiri ya kubadilishiwa mkuu huyo wa kituo lakini imekuwa patupu.
Wananchi walimaliza kusema kuwa kutokana na mtaa wao kuhitaji
mkuu wa kituo mwenye kichwa ngumu na mchapakazi wameliomba Jeshi hilo
kumrejesha aliyewahi kuwa mkuu wa kituo hicho Sajent Chalo ambae aliweza
kusambaratisha uharifu wote kiasi cha vijana wengi kustaafa uharifu na
kujiingiza kwenye vikundi vya biashara ili kujipatia pesa kwa njia harali.
Aisha
Sajent Chalo pia alikuwa na mbinu za kisasa za kuondoa uharifu ni pamoja na
kukaa vikao mara kwa mara na vijana hao wa kihuni na kuwasihi kaucha uharifu
hali iliyozaa matunda na sasa wamemuomba Kamanda Wambura kufanya jitihada za
kumrejesha Sajent Chalo haraka ili kunusuru hali ya usalama katika eneo hilo.






.jpg)
0 comments:
Post a Comment