Mh.mtarajiwa Shilole akifanya vitu vyake maskanibongotz
Mh. Shilole kama anavyoonekana
Mh. Mtarajiwa Manaiki Sanga the Don
Manaiki Sanga
Na Sakina Shabani
Muamko wa vijana kujiunga na siasa unazidi kushika kasi ambapo mtandao huu wa maskanibongotz ina majina kumi ya wasanii wa muziki wa bongo flava na bongo movie wanaosadikika kutangaza nia ya kugombea Ubunge kwenye majimbo mbalimbali nchini.
Maskanibongotz ina data hizo kuwa wasanii hao ambao wako waliweka wazi ishu hiyo na wako wanafanya siri hadi siku ikifika na msanii Judith Wambura ambae mwanzoni mwa mwaka huu alionekana kuchukua kadi kupitia chama cha Chadema lakini hadi sasa haijafahamika kama anagombe wapi ila kuna tetesi kuwa atagombe kwenye moja ya majimbo ya Jijini Dar.
Profesor J: Nae hivyo hivyo amejiunga na Chadema pia kuna tetesi atagombea jimbo moja lililopo Mkoa wa Pwani.
Msanii Kingwendu: Tayari ametangaza nia bila kuhamika kupitia chama ganio lakini jimbo lipo Temeke
Manaiki Sanga: Huyu ametangaza ni kupitia Chama Cha CCM huko Iringa huku jimbo likiwa siri yake
Shilole: Yeye ameweka wazi kuwa anataka kumng'oa Mh Rage kule Tabora na kiti hicho anakitaka bila kubainisha kupitia Chama gani
Roma: Mwanamuziki huyu kipenzi cha maelfu ya wananchi hasa vijana ametangaza nia pia ya kugombea Ubunge kupitia CHADEMA bila kuweka wazi jimbo.
JB: Pia ametangaza nia siku nyingi anasubiri muda ufike tu aanze harakati ingawa haifahamiki ni jimbo gani atagombea.
CREDIT: MASKANIBONGOTZ
0 comments:
Post a Comment