Wednesday, November 5, 2014

UKATILI MKUBWA: MWIZI ACHEZEA KICHAPO KISHA ANYWESHWA MAJI YA CHOONI LITA 3 KISHA KURUHUSIWA KURUDI KWA MKEWE..!


 Kijana aliyefahamika kwa jina la Chota Msimbe ambae ni mwizi chipukizi anaejifunza kuiba, hapa akilia kwa uchungu na kuomba asamehewe asiuliwe kwa vile alikuwa najifunza kuimba na siku hiyo ilikuwa mara ya kwanza.
Maji machafu ya chooni
Na Sakina Shabani-Maskanibongotz
Kijana mmoja ambae ni mwenyeji wa Mkoa wa Morogoro lakini anaishi Jijini Dar hivi karibuni alifanyiwa ukatili wa kutisha baada ya kunyweshwa maji ya chooni zaidi ya lita tau kufuatia kujaribu kumuibia Mama mmoja simu maeneo ya Uhuru Kariakoo.
Kamera za Maskanibongotz zilinasa tukio hilo la kusikitisha ambapo kijana huyo ambae kwa mujibu wa watu wanaomfahamu walisema anajifunza uwizi hivyio hata siku hiyo ilikua simu yake ya kwanza kuimba lakini akanaswa, hata hivyo siku ya tukio kijana huyo alikuwa najaribu kumuibia mama mmoja simu kwenye kipima joto chake lakini akaishia kunaswa na wananchi wenye ghazabu walianza kufanya yao kwa kumgombea kama mbwa mwizi.
Hata hivyo wakati wananchi wakiendelea kumsulubu kijana huyo alisikika akisema kuwa anaomba asemehewe kwa vile alikuwa ana jifunza na ameamini uwzi sio mzuri hivyo siku hiyo ilikuwa mwanzo na mwisho na aliahidi atakua balozi mzuri kwa vijana wote wanaotaka kujiingiza kwenye uwizi na atawambia haufai.
Kijana huyo aliongeza kujitetea kuwa kama watamuua hawatasaidia ni heri wamuache akawakanye wenzake, hata hivyo maneno hayo ya busara yaliwaingia watu ambao waliamua kumsamehe lakini walimwambia wampe adhabu kidogo ambapo walichota walichota maji ya mataroni yanayotka chooni kama lita tatu na nusu na kumnywesha yote kisha wakamruhusu arudi kwa mkewe mmh.
CREDIT: MASKANIBONGOTZ

0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king