Maelfu ya watu wakiwa kwenye mihadhara ya Shekh Sharif Khamisi nchini Kongo, ambapo kijana huyo wa Tanzania yupo huko kwa mwaliko wa wananchi wa huko kwa ajili ya kuombea Amani
Nchi ya Kongo imeendelea kushtushwa na maajabu anayoyafanya kijana wa kitanzania Shekh Sharif Khamis raia wa Tanzania baada ya hivi karibuni kufanya maajabu ya kutisha baada ya kuendesha meli wakati hajawahi kusomea urubani hata siku moja.
Kwa mujibu wa gazeti moja la Serikali nchini humo ilisema kuwa Rais Kabila ambae anaiongoza nchi yenye mahusiano mazuri na Tanzania ameshtushwa sana na taarifa za kijana huyo huku nae akimpongeza kwa jitihada za kijana huyo kuiombea dua njema nchi yake.
Habari zaidi zilisema kuwa Shekh Sharif Khamis amekuwa akijaza watu katika hadhara zake kiasi cha kuogopesha huku watu mbalimbali wakiombewa dua wakiwemo waasi pamoja na wachimba madini.
Kijana huyo bado yupo nchini humo hadi mwisho wa mwaka huu kabla ya kurudi nchini kwa kujiandaa na safari ya kuelekea nchi zenye machafuko kama Syria, Libya, Misri, Iraq na Israel.
0 comments:
Post a Comment