Wednesday, November 5, 2014

MISS RUVUMA MATATANI KWA KUMSHAMBULIA MWANDISHI WA HABARI WA 93.7 E-FM RADIO!

 Bw. Livingstone Mkoi mwandishi wa habari wa 93.7 E-FM RADIO na mkurugenzi mtendaji wa Gazeti la Maskanibongo
 Kalama na Isabela Mpanda ambae anatafutwa kwa tuhuma hizo
 Livingstone Mkoi kushoto akiwa kazini na wanahabari wenzake wakitimiza majukumu yao


Na Salim Ramadhan
Miss zilipendwa 2007 toka Ruvuma Isabelah Mpanda ameingia anga mbaya baada ya kumtukana matusi mazito mwandishi wa habari wa kituo kipya cha radio cha E-fm 93.7,  Bw Livingstone Mkoi.
Miss Ruvuma huyo ambae kwa sasa ni mwanamuziki amedaiwa kutenda kosa hilo usiku wa tarehe 4 kuamikia tareh 5 mwezi huu baada ya kuandika ujumbe wa maneno ya kumkashfu mwandishi huyo pamoja na kumtukana matusi mazito bila kufahamika sababu za msingi.
Hata hivyo kwa mujibu wa mwandishi huyo aliuambia mtandao huu kuwa siku ya Jumanne asubuhi wakati akijiandaa kuelekea kwenye majukumu yake ya ujenzi wa taifa alipokea simu toka kwa watu wake wa karibu wakimpatia pole huku yeye akishangaa kulikoni kwa pole hizo.
Baada ya kuelezwa kulichotokea mwandishi huyo aliingia mtandaoni na kujionea udhalilishaji huo wa matusi ya nguoni huku pia mrembo huyo akiweka picha ya mwanahabari huyo ambae pia ni mkurugenzi mtendaji wa Gazeti la Maskani Bongo.
Kufuatia mambo hayo mwanahabari huyo alienda kutuoa taarifa Polisi kituo kidogo cha Polisi kilichopo Kinondoni Moscow ambapo walimfungulia jalada KH/RB/1132/2014 KUDHALILISHA KUTUMIA MTANDAO/ MATUMIZI MABAYA YA MTANDAO na tayari jalada hilo limetua Oysterbay Polisi kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Aidha mwandishi alipouulizwa kama ana ugomvi wowote na mrembo huyo alisema “ Hapana sikuwa kuwa na ugomvi nae namheshimu  kama dadangu na huwa nashirikiana mambo mengi kiukweli sielewi imekuaje yani” Alisema Mkoi
Mtandao huu ulimtafuta Mrembo huyo ili aelezee tuhuma hizlo lakini simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa hadi news hii inaruka hewani kama hivi.


0 comments:

Post a Comment

.

 

Copyright © MASKANI BONGO Design by Livingstone Mkoi | Blogger Theme by BTDesigner | Powered by seleman king